Friday, 30 August 2013
Zitto Kabwe: Msiwaamini wanasiasa, chama tawala wala wapinzani
Kauli hii ameitoa leo katika kongamano la ufuatiliaji wa uwajibikaji Jamii ambapo yeye alikuwa akiongelea majukumu ya bunge katika kusimamia uwajibikaji.
Mambo mengi aliyoongea yalikuwa ni yenye mwelekeo chanya isipokuwa hili la kutupa tahadhari ya kutowaamini wanasiasa, akisisitiza hata wa upinzani.
Nyuma ya kauli hii kumejificha nadharia nyingi kutegemea na mtu atakavyoipokea.
Kwa maana nyingine, kauli hii inaleta hisia kwamba, hata wale wa chama chake tusiwaamini pia.
Kwa kuwa mheshimiwa ni miongoni mwa members hapa, najua ujumbe huu utamfikia. Nilitaka atoe ufafanuzi alikuwa anamaanisha nini kwa kauli yake hii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment