Thursday, 15 August 2013

SAKATA LA MADIWANI BUKOBA: MWENYEKITI WA CCM MKOA ATOFAUTIANA NA NAPE

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera, Bi. Constansia Buhiye leo amesisitiza kuwa maamuzi yaliyotolewa na Halmashauri kuu ya Mkoa ya kuwafukuza na kuwaondolea nyadhifa madiwani wanane wa chama hicho Manispaa ya Bukoba yako palepale.

Akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa CCM
kuhusiana na Tamko la Katibu Mwenezi Taifa Ndugu Nape Nnauye la kutengua maamuzi ya Halmashauri kuu ya Mkoa wa Kagera, Bi Buhiye amesema hata taarifa ya Nape hajaisikia, na kwamba  maamuzi waliyoyafanya ni kwa mujibu wa Katiba ya Chama.
Mwenyekiti wa CCM mkoa Kagera akiongea na waandishi wa habari leo kususitiza kuwa  maamuzi ya halmashauri kuu ya mkoa dhidi ya madiwani  wanane wa CCM  Bukoba yako palepale
  Waandishi wa habari wakisikiliza maelezo ya mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera leo

0 comments:

Post a Comment