Sunday, 25 August 2013

TAARIFA ZA KUKAMATWA VIONGOZI WA CHADEMA IRINGA

VIONGOZI waandamizi wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Taifa akiwemo mwenyekiti wao Bw Freema Mbowe, Mbunge wa Singida Mashariki ambae ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Tundu Lissu na mwenyeji wao mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa wakamatwa na polisi mkoani Iringa Viongozi hao  wamekamatwa   leo majira ya saa 3 asubuhi kati kati ya mji wa Iringa wakati wakitokea eneo la Kihesa kuelekea Bungeni mjini Dodoma kwa shughuli za kibunge kabla ya jeshi la polisi kuwatia matatani na kuwafikisha kituo cha polisi .
 Akithibitisha kukamatwa viongozi hao kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi alisema kuwa viongozi hao walikamatwa kwa mahojiano kutokana na kutoa kauli hatarishi kwa amani wakati wa mkutano wao uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa kwa ajili ya mabaraza ya ukusanyaji wa maoni ni rasmu ya katiba.
 Kamanda Mungi alisema kuwa kibali ambacho Chadema walipewa kilikuwa kikianza saa 9 Alasili hadi saa 12 .;00 ila wao waliendelea na mkutano huo hadi majira ya saa 12 .25 na kila walipofuatwa zaidi ya mara moja kuelezwa kuhusu muda wa kibali chao kuisha bado viongozi hao waliendelea kuendesha mkutano huo huku wakitumia vipasa sauti kutoa maneno ya dhahaka dhidi ya jeshi la polisi

0 comments:

Post a Comment