NAPE AWAPONDA CHADEMA
- .Adai wanawapotezea watu muda mikutano ya Katiba
- Ajivunia utaratibu uliotumiwa na CCM
- Adai wanachofanya Chadema ni uhuni
Katibu wa
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye
amewaponda Chadema na utaratibu wanaotumia kukusanya maoni ya wananchi
juu ya rasimu ya kwanza ya katiba kuwa ni uhuni na kuwapotezea watu muda
Nape
akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma alipokuwa akielezea
ratiba ya vikao vya CCM vya kitaifa alisema,"sisi tunakutana kupitia
maoni ya wanaCCM waliotoa maoni yao juu ya rasimu ya kwanza ya katiba,
lakini wakati sisi tunafanya hivyo watani zetu wameamua kuwapotezea muda
wananchi kwa kufanya uhuni wa mikutano ya hadhara huku wakijua kuwa ni
kinyume na sheria inayoongoza mijadala ya rasimu hiyo ya
katiba"alisisitiza Nape.
Lakini
Nape pia alimpongeza mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya katiba nchini
Jaji Warioba kufuatia kauli yake kuwa atapokea maoni ya taasisi sio ya
helkopta.
"Jaji
warioba kawatendea haki hawa watani, sheria inataka taasisi ikae kama
baraza sio ikafanye mikutano ya hadhara.Kasema sawa sawa, hawatapokea
maoni ya helkopta ila ya taasisi sasa sio busara hawa jamaa kuendelea
kupoteza muda wa watu".
"Lakini
najua wataendelea tu kwasababu inabidi watoe hesabu ya pesa walizopewa
kwa kazi hii.Watafanyaje sasa zaidi ya kuruka na chopa ili wakidhi
matakwa ya waliowatuma,ndo tabu ya vibaraka!"alisisitiza Nape.
Kuhusu
vikao alisema sekretariete ya CCM imekutana kwa siku tatu mjini Dodoma
kuandaa kamati kuu inayokutana kesho na Halmashauri kuu inayokutana
tarehe 24 -25/08/2013.
0 comments:
Post a Comment