Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin
Yusuph akipolewa na Mwalimu wa Taalum na msimamizi wa Maktaba wa Shule
ya wasichana ya Mwedo, Joseph Mangomes alipofika shuleni hapo kukabidhi
msaada wa vitabu vya masomo ya Sayansi uliotolewa na Shirika la Read
International kupitia UNESCO.
Na Mwandishi wetu, Arumeru
Wanafunzi wa shule ya Mwedo sekondari iliyopo wilayani Arumeru
wamelishukuru Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kupitia
Read International la nchini Uingereza kwa kuweza kuwapatia vitabu vya
kiada vya masomo ya Sayansi hali itakayowafanya kupiga hatua katika
masomo hayo.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi hao Kaimu mkuu wa shule hiyo Clara
Meijo alisema kuwa kutokana na changamoto mbalimbali za masomo ya
Sayansi wanalishukuru Shirika la Read International kwa kuweza kuwapatia
vitabu hivyo tulivookabidhiwa na UNESCO.
Meijo alisema kuwa shule hiyo ilianzishwa mwaka 2011 ikiwashirikisha
wasichana wa kimasai wanaoishi katika mazingira magumu wakiwa ni
wanafunzi waliokosa nafasi ya kupata elimu kwa kuwachukua wanafunzi
kutoka maeneo mbalimbali kwenye jamii ya kifugaji.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin
Yusuph (kulia) akisalimiana na Mwalimu Clara Meijo mara baada ya
kuwasili shuleni hapo.
Aidha alisema kuwa wanafunzi hao ni wale waliokuwa kwenye maeneo ambayo
upatikanaji wa elimu yalikuwa mbali, shule hiyo inayomilikiwa na Shirika
la Wanawake wa Kimasai (MWEDO) lenye makao makuu yake jijini Arusha
huku shule hiyo ikiwa imejengwa kwa michango mbalimbali ya wafugaji kwa
kutoa mifugo yao.
“Changamoto kubwa inayoikabili shule yetu ni upungufu wa mabweni, maji
na umeme wa kudumu ikisababisha wanafunzi kushindwa kujianda kwa
mitihani yao kwa kujisomea nyakati za usiku hali inayoangusha ufaulu kwa
wanafunzi hao” alisema Meijo.
Ameiomba Serikali na wafadhili kuwasaidia kupata umeme kwa haraka
ilikuweza kuongeza ufaulu na idadi ya wanafunzi huku akiomba pia
kusaidiwa upatikanaji wa maji safi kwenye shule hiyo na kuongeza kuwa
msaada huo wa vitabu umekuja wakati muafaka kwao na utasaidia kukua kwa
ufaulu shuleni hapo.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin
Yusuph akisaini kitabu cha wageni shuleni hapo. Kulia ni Afisa Mradi wa
uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai (GEBR) Kitengo cha Sayansi kutoka
UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko aliyeambatana na Bw. Al
Amin.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin
Yusuph alisema kuwa wanaimani kubwa kuwa vitabu hivyo vitatumika
kuongeza uelewa kwa wanafunzi na kuwa vitabu hivyo vinatambuliwa na
Wizara ya Elimu katika kufundishia masomo ya Sayansi hivyo ni wajibu
wenu kama wanafunzi kujifunza kwa bidiii ili muwe mabalozi wazuri katika
ujenzi wa taifa.
Bw. Al Amin aliongeza kuwa wanampango wa kuiboresha maktaba ya shule
hiyo kwa kuongeza matumizi ya Tehama kwa upatikanaji wa taarifa
mbalimbali kwa ajili ya masomo.
Shule hiyo inawafanyakazi 18 wakiwemo walimu kumi na idadi ya wanafunzi
wakiwa 153 huku wanafunzi kumi ni wakutwa na waliobakia ni wa bweni.
Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA,
Myoung Su Ko akisaini kitabu cha wageni shule ya sekondari ya wasichana
ya Mwedo iliyopo wilayani Arumeru jijini Arusha.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin
Yusuph (kulia) akizungumza na Mwalimu wa Taalum na msimamizi wa Maktaba
wa Shule ya wasichana ya Mwedo, Joseph Mangomes (wa pili kulia) wakati
akikagua maktaba ya shule hiyo kabla ya kukabidhi msaada wa vitabu vya
masomo ya sayansi vilivyotolea na Shirika la Read International kupitia
UNESCO. Kutoka kushoto ni Mwalimu Clara Meijo, Afisa Mradi wa Shirika la
Wanawake wa Kimasai (MWEDO) liliojenga shule hiyo Martha Sengeruan na
Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA,
Myoung Su Ko.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin
Yusuph akitoa maelekezo ya namna ya upangiliaji wa vitabu kwenye maktaba
hiyo kwa Mwalimu wa Taalum na msimamizi wa Maktaba wa Shule ya
wasichana ya Mwedo, Joseph Mangomes.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin
Yusuph (wa pili kulia) akipitia rekodi za uhifadhi wa maktaba hiyo kabla
ya kuwaahidi kuleta Kompyuta itakayokuwa "Software" ya kisasa zaidi na
kuweza kuwarahisisha kuhifadhi na utunzaji wa kumbukumbu za maktaba
hiyo.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin
Yusuph (kulia) akisikiliza maelezo ya mwanafunzi Evaline Gerald wa
kidato cha pili shuleni ya sekondari ya wasichana MWEDO anayesaidiana na
Mwalimu wake katika kutoa huduma za maktaba ya shuleni hapo.
Sehemu ya mashelfu ya kuhifadhia vitabu kwenye maktaba ya shule hiyo.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin
Yusuph (kulia) na fisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na
mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko wakipata maelezo ya maabara ya shule y
sekondari ya wasichana MWEDO kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Sayansi
shuleni hapo Bw. Edickiel Mturi.
Mwalimu wa Taalum na msimamizi wa Maktaba wa Shule ya wasichana ya
Mwedo, Joseph Mangomes akiutambulisha ugeni wa UNESCO kwa wanafunzi na
walimu wa shule ya sekondari ya wasichana MWEDO wakati wa hafla ya
kukabidhi msaada wa vitabu shuleni hapo.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin
Yusuph, akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya
MWEDO wakati wa halfa ya kukabidhi vitabu vilivyotolewa na Shirika la
Read International kupitia UNESCO ambao aliwaasa wanafunzi hao kusoma
kwa bidii kuweza kukomboa familia zaidi hapo baadae kupitia elimu.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin
Yusuph akionyesha baadhi ya vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolewa
na Shirika la Read International kupitia UNESCO. Kulia ni Afisa Miradi
Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin
Yusuph, akikabidhi sehemu ya msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi kwa
Mwanafunzi Evaline Gerald wa kidato cha pili shule ya sekondari ya
wasichana MWEDO uliotolewa na Shirika la Read International kupitia
UNESCO. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi
kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko (kulia) na kushoto ni
Afisa Mradi wa Shirika la Wanawake wa Kimasai (MWEDO) liliojenga shule
hiyo, Martha Sengeruan.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin
Yusuph, Walimu na Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja
mara baada ya kukabidhiwa msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi
vilivyotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya MWEDO
wakishusha maboksi yaliyosheheni vitabu vya masomo ya sanyansi
vilivyotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO. Source VIJIMAMBO
0 comments:
Post a Comment