Songea.
Polisi mkoani Ruvuma wanamshikilia mtoto wa miaka 15 (jina limehifadhiwa), mkazi wa Makambi mjini hapa kwa tuhuma za kuwalawiti watoto wenzake sita katika nyakati tofauti.
Watoto wanaodaiwa kulawitiwa na kijana huyo wana umri chini ya miaka 10.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Kamishna
Msaidizi wa Polisi, Mihayo Msikhela alisema matukio hayo yalitokea kati
ya Julai 30 na Agosti 3 mwaka huu.
Alisema kati ya watoto waliolawitiwa, watano ni wanafunzi wa Shule ya Msingi Majimaji na mmoja wa Shule ya Skill Path.
Mmoja wa wazazi wa watoto hao ndiye aliyegundua kuwapo kwa vitendo hivyo na kutoa taarifa kituo cha polisi Songea.
Kamanda Msikhela alisema mtuhumiwa huyo alikuwa
akiwadanganya watoto kwa kuwapa Sh100 au miwa aliyokuwa akiuza karibu na
nyumba chakavu aliyokuwa akifanyia kitendo hicho.
Katika kufanikisha matendo hayo, mtuhumiwa anadaiwa kuwatisha watoto hao kwa kuwapiga fimbo endapo wangetoa taarifa.
Mmoja wa wazazi wa mtoto aliyelawitiwa walibaini
hali hiyo baada ya kuona mabadiliko ya mtoto wao na walipombana alikiri
kuingiliwa na mtuhumiwa huyo.
Baada ya kutiwa nguvuni, mtuhumiwa alikiri kuwafanyia kitendo hicho watoto wenzake.
“Amekiri kuhusika, tunafanya uchunguzi kabla ya kumfikisha mahakamani kujibu mashtaka,” alisema Kamanda.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa
Songea, Lucy Ngoi amethibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kwamba watoto
waliofanyiwa vitendo hivyo wanaendelea na vipimo kubaini kama kuna
wameambukizwa maradhi yoyote. Chanzo MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment