Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya
watu duniani (UNFPA), Dkt Natalia Kanem akizungumza wakati wa
maadhimisho hayo ya siku ya kimataifa ya vijana duniani kwenye viwanja
vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Kushoto ni Mgeni Rasmi kutoka
Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Bibi Venerose Mtenga na
kulia ni Mtaalamu wa Programu za Vijana kutoka UNFPA, Tausi Hassan.(
Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
.Siku ya vijana duniani na ujumbe wa “Vijana na Afya ya Akili”
.Takwimu zinaonyesha nusu ya idadi ya watu nchini ni vijana
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI Kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo imeahidi
kukuza na kuboresha misingi ya kuwashirikisha vijana katika utekelezaji
wa sera mbalimbali, programu na mikakati ya maendeleo.
Akisoma hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni,
Vijana na Michezo, Bibi Sihaba Nkinga, wakati wa maadhimisho ya siku ya
vijana duniani kwenye viwanja vya Chuo Kikuu Dar es Salaam, Bibi
Venerose Mtenga amesema kwamba lengo la kuwashirikisha vijan ni
kuhakikisha kuwa sauti zao zinasikika na kufanyiwa kazi.
“Katika kutekeleza eneo hili Tanzania inalenga kuweka fursa
zitakazowawezesha vijana kukuza utaalamu na ujuzi utakaowawezesha
kufanikiwa katika kipindi cha mpito kutoka ujana kwenda katika utu
mzima,” amesema Bibi Mtenga.
Amesema kwamba Tanzania kama sehemu ya dunia inatambua changamoto maalum
zinazowakabili vijana walioko katika mazingira hatarishi pamoja na
umuhimu wa kuhakikisha kuwa vijana wanahusishwa kikamilifu katika
malengo ya maendeleo.
Bi Mtenga aliongeza Tanzania itaendelea kufanya kazi kwa karibu na
vijana pamoja na wadau wa maendeleo ili kuunga mkono programu za elimu
ya afya kwa vijana walioko ndani na nje ya shule.
Alilisitiza kwamba Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo
wataendelea kuunga mkono taasisi za mafunzo rasmi na zisizo rasmi ili
kukuza uwezo na uelewa miongoni mwao katika masuala ya afya ya akili na
mwili kwa ujumla.
“siku ya vijana duniani inatambua na kuthamini kuwa kipindi cha ujana
kinaambatana na mabadiliko makubwa na ya haraka na safari ya kutoka
utotoni kufikia utu mzima,”
“Safari hiyo inaweza kuwa ngumu na yenye changamoto nyingi na hivyo
kuhitaji utulivu na ukomavu wa akili, hapa Tanzania, kwa mujibu wa Sera
ya Taifa ya Maendeleo ya vijana, kijana ni mtu yeyote mwenye umri kati
ya miaka 15 hadi 35,” aliongeza
Amesema kwamba katika takwimu za kitaifa hapa nchini nusu ya idadi ya
watu ni vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa na uchumi wa nchi kwa
ujumla.
Mgeni Rasmi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Bibi
Venerose Mtenga akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ya siku ya
kimataifa ya vijana duniani, kushoto kwake, ni Mwakilishi wa UNFPA, Dkt.
Natalia Kanem.
Bibi Mtenga aliendelea kusema kwamba msisitizo mkubwa unawekwa katika
kuhakikisha vijana wanakuwa na fikra chanya ambazo ni za kimaendeleo na
zinazoleta mabadiliko chanya kwa jamii.
Kwa Upande wake, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem
amesema kwamba siku ya vijana duniani ni nafasi nyingine kwa vijana
kukutana pamoja na kujadiliana matatizo na changamoto mbalimbali
wanazokabiliana nazo.
Amesema kwamba vijana kwa kushirikiana na makundi mbalimbali ya kitaifa
na kimataifa katika kupambana na changamoto za matumizi ya pombe kupita
kiasi, dawa za kulevya na mimba za utotoni.
“kwa pamoja serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika ya
kimataifa wana wajibu wa kushirikiana na vijana katika kuwasaidia
kufikia malengo yao mbalimbali katika harakati za kujiletea maendeleo,”
amesema Dkt. Kanem.
Baadhi ya timu za mpira wa kikapu na wanafunzi kutoka shule mbalimbali
za sekondari nchini wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya
siku ya kimataifa ya vijana duniani.
Dkt Kanem aliongeza kwamba ni muhimu kwa vijana kutambua kwamba bila
kuwa na afya nzuri ya akili ni vigumu kupiga hatua za kimaendeleo na
kuondokana na umaskini wa kipato.
Amesema kwamba katika mkutano unaokuja wa viongozi duniani watatumia
nafasi hiyo kuwakumbusha viongozi wa dunia umuhimu wa kuwekeza kwa
vijana kama taifa la kesho.
Dkt.Kanem alifafanua umuhimu wa vijana na jamiii kwa ujumla kutumia
mitandao ya kijamii katika kupashana habari za afya ya uzazi na mambo
yanayowahusu vijana kwa ujumla.
Wakati huo huo, Katika mashindano ya mpira wa kikapu timu zilizoshiriki
ni timu saba kati ya hizo tano ni za wanaume na pili za wasichana.
Kwa upande wa wasichana mshindi wa kwanza ni Don Bosco Lioness na
washindi wa pili ni Tanzania Prisons Queens na kwa upande wa wavulana,
washindi wa kwanza Lord Baden-Powell Memorial High School, washindi wa
pili Makongo High School, washindi wa tatu ni Kizuka Sekondari school.
Timu zilizoshiriki ni Tanzania Prisons Queens, Lord Baden-Powell
Memorial High School, Makongo High School, Don Bosco Lioness, Kizuka
Sekondari School, Tabata Segerea na Bahari Beach.
Mgeni rasmi, Venerose Mtenga akirusha mpira wa kikapu kuzindua rasmi
mashindano ya mchezo wa mpira wa kikapu kwa vijana wa shule za sekondari
nchini wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani.
Mwakilishi wa UNFPA, Dkt Natalia Kanem akirusha mpira wa kikapu
kuashiria uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana
duniani.
Mgeni Rasmi na Mwakilishi wa UNFPA wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya timu za mpira wa kikapu.
Mgeni rasmi, Venerose Mtenga akiwa katika picha ya pamoja na timu ya
wasichana ya mpira wa kikapu wakati wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya
vijana duniani.
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia
Nkhoma Ledama (kulia) na Mgeni rasmi, Venerose Mtenga (kushoto)
wakimuonyesha jambo Mwakilishi wa UNFPA, Dkt Natalia Kanem (katikati)
mara baada ya kupata picha za kumbukumbu na timu zilizoshiriki bonanza
hilo la mpira wa kikapu katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya vijana
duniani.
Mwakilishi wa UNFPA, Dkt Natalia Kanem akisalimiana na msanii muziki wa
bongo flava Domokaya (wa pili kulia) wakati wa maadhimisho ya siku ya
kimataifa ya vijana duniani.
Mtaalam wa Mawasiliano kutoka UNFPA, Sawiche Wamunza akipata u-selfie na
msanii wa bongo flava Domokaya wakati wa maadhimisho hayo.
Phillip Musiba kutoka kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC)
akipata picha na msanii wa muziki wa bongo flava nchini Domokaya.
Timu za Kizuka sekondari kutoka Morogoro, (Nyeupe) na Makongo Sekondari
(Njano) wakitoana jasho katika mchezo wa ufunguzi wa mpira wa kikapu,
Makongo walishinda vikapu 30 dhidi ya 14 ya Kizuka sekondari kutoka
Morogoro.
Mgeni Rasmi, Bibi Venerose Mtenga akifafanuliwa jambo kutoka kwa Mshauri
wa vijana, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu
duniani (UNNFPA), Bw, John Kalimwabo alipotembelea banda hilo.
Mgeni Rasmi, Bibi Venerose Mtenga akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu
Tatu Mwakifuna na Mwanafunzi wake, Zawadi Salehe wote kutoka KIWOHEDE.
Kushoto kwa mgeni rasmi ni Mtaalamu wa Programu za Vijana kutoka UNFPA,
Tausi Hassan.
Mgeni rasmi akipata maelezo kutoka kwenye banda la Tanzania Network
Against Alcohol Abuse kwenye moja la shirika lake la Tanzania Girl
Guides Association, anayetoa maelezo ni Fadhia Khamis Ally na kushoto
kwake ni Shadya Soud Milanzi wasichana hao wanatoka Girl Guides ambacho
ni chama kisicho cha kiserikali na ni chama cha kujitolea, madhumuni
yake ni kuwaendeleza wanawake pamoja na motto wa kike katika maswala ya
kijamii na kiuchumi kwa kuwapa elimu na mafunzo.
Mgeni rasmi, Bibi Venerose Mtenga akimsikiliza kijana kutoka Kituo cha
Vijana UMATI, Temeke, Kassim Abdallah alikuwa akimweleza mgeni rasmi
jinsi wanavyotoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana kwa kutumia
vipeperushi na ushauri nasaha.
Wawakilishi kutoka Marie Stopes Hospital Tanzania, Bibi Zayana Nuhu na
John Basso Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wakimweleza jambo mgeni rasmi
jinsi hospitali hiyo inavyofanya kazi hapa nchini.
Mgeni rasmi akipata picha ya kumbukumbu na mmoja wa wahudumu wa banda la Marie Stopes wakati wa maadhimisho hayo.
Joynes Ashery kutoka Marie Stopes Hospital Tanzania akifafanua jambo
kuhusiana na masuala ya afya ya uzazi kwa Afisa Habari wa Kituo cha
Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) ambao ni wameshiriki kuratibu
maadhimisho hayo, Stella Vuzo.
Mshauri wa vijana, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi
ya watu duniani (UNNFPA), Bw, John Kalimwabo akitoa maelezo ya matumizi
sahihi ya Kondomu za kike kwa kutumia kiungo bandia cha mwanamke kwa
vijana waliohudhuria maadhimisho ya kimataifa ya siku ya vijana duniani.
Vijana wakiendelea kumiminika kwenye banda ya UNFPA kupata maelezo
mbalimbali wakati wa maadhimisho ya kimataifa ya siku ya vijana duniani
yaliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM).
Mratibu wa uzazi wa mpango kutoka shirika la PSI, Hadija Ameir akitoa
elimu ya uzazi wa mpango kwa vijana wakati wa maadhimisho hayo katika
viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella
Vuzo akizungumza na baadhi ya watoto walioshiriki mashindano ya kuchora
picha mbalimbali zikiwemo za kuhamasisha vijana kuachana na matumizi ya
madawa ya kulevya baada ya kuvutiwa na kazi zao.
Mtoto Tarzan Iddy akionyesha picha yake aliyoichora ikizungumzia uvutaji wa Bangi kwa vijana.
Mgeni rasmi, Bibi Venerose Mtenga na Afisa Habari wa kituo cha Habari
cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama wakikagua baadhi ya
picha hizo na maudhui kabla ya kutangaza washindi.
Mgeni rasmi, Bibi Venerose Mtenga akikabidhi nyenzo za sanaa ya uchoraji
zilizotolewa na UNFPA kwa mtoto Lawrence Dennis wakati wa maadhimisho
ya kimataifa ya siku ya vijana duniani.
Mgeni ramsi Bibi Venerose Mtenga akimkbidhi mmoja kati ya tatu bora wa
mashindano ya uchoraji Aziza Iddy nyenzo za sanaa ya uchoraji kutoka kwa
zilizotolewa na UNFPA sambamba na ufadhili wa kusomeshwa kulipiwa ada
ya darasa la uchoraji kwa siku tano.
Mgeni ramsi Bibi Venerose Mtenga akiwavalisha medali timu zilizochukua ubingwa wakati wa maadhimisho hayo.
Mgeni ramsi Bibi Venerose Mtenga akimkabidhi zawadi Kaimu Katibu Mkuu wa
Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) Michael Maluwe kama
shukrani ya kuratibu bonanza la mpira wa kikapu kwa vijana wakati wa
maadhimisho hayo.
Mgeni ramsi Bibi Venerose Mtenga akiwa kwenye picha ya pamoja na
washindi wa kwanza wa bonanza la mpira wa kikapu timu ya Lord
Baden-Powell.
Timu ya wasichana ya mpira wa kikapu ya Don Bosco Lioness kwenye picha ya pamoja na Mgeni ramsi Bibi Venerose Mtenga.
Timu ya waichana ya Don Bosco Lioness wakijipiga u-selfie baada ya kuibuka kidedea kwenye maadhimisho hayo. ChanzO VIJIMAMBO