Jeshi la
Ulinzi la Kenya liliwatia mbaroni Watanzania watatu ndani ya Somalia
wakiwashuku kuwa walikuwa njiani kwenda kujiunga na Al-Shabaab, gazeti
la The Standard la Kenya liliripoti siku ya Jumapili (tarehe 20 Oktoba).
Ali Ramadhan
mwenye umri wa miaka 22, Musa Daudi miaka 19 na Shabaan Bakiri Waziri
miaka 21, walitiwa mbaroni baada ya kuingia Somalia kutoka Kenya na sasa
wanahojiwa katika kituo cha polisi cha Kiunga.
Polisi
walisema kwamba washukiwa hao walitokea Dar es Salaam, wakasafiri hadi
mpaka wa Tanzania na Kenya huko Lungalung, baadaye wakaenda kwa gari
hadi Mombasa, Malindi na Lamu kabla ya kuingia Somallia.
Kwa mujibu
wa polisi, watatu hao walikuwa wanaelekea Kismayu kwenda kujiunga na
"vita vitakatifu, walivyodai vinaongozwa na [Al-Shabaab]".
0 comments:
Post a Comment