Nairobi, Kenya. Wanajeshi wawili
nchini Kenya wamefutwa kazi na kufungwa jela kwa kitendo cha kupora mali
wakati wa shambulizi la kigaidi kwenye Jengo la Westgate mwezi jana.
Hayo yamesemwa na mkuu wa jeshi la Kenya, Julius Karangi.
Karangi amesema kuwa mwanajeshi wa tatu aliyeshukiwa kwa uporaji anachunguzwa.
Awali Karangi alikanusha kuwa
wanajeshi walifanya uporaji kwenye jengo hilo licha ya picha za CCT
kuonyesha wanajeshi wakibeba mifuko ya plastiki kutoka kwenye moja ya
maduka makubwa yaliyokuwa ndani ya Jengo la Westgate.
Hivi karibuni wanamgambo wa Somalia,
al-Shabaab walikiri kufanya shambulizi hilo na kuwateka nyara Wakenya
kadhaa waliokuwa ndani ya jengo hilo kwa siku nne.
Watu 67 walifariki na mamia ya wengine kujeruhiwa.
Wakati huohuo, mkuu wa kitengo cha
uchunguzi wa uhalifu katika idara ya polisi,Ndegwa Muhoro alisema kuwa
mmoja wa magaidi waliokuwa ndani ya jengo hilo walipiga simu nchini
Norway wakati walipovamia jengo hilo.
Mmoja wa washukiwa wa shambulizi hilo ametajwa kuwa Hassan Abdi Dhuhulow mzaliwa wa Somalia ambaye ana uraia wa Norway.
Jeshi limesema kuwa magaidi wote wanne waliofanya shambulizi hilo waliuawa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment