Saturday, 19 October 2013

AKINA SAMATTTA, ULIMWENGU NA MAZEMBE WATINGA FAINALI AFRIKA

BAO pekee la Tressor Mputu dakika ya saba, limeipa ushindi wa 1-0 Tout Puissant Mazembe dhidi ya Stade Malien ya Mali katika Nusu Fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi leo.
Matokeo hayo yanaifanya Mazembe yenye washambuliaji wawili Watanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu itinge fainali ya michuano hiyo.
Hata hivyo, bado haijajulikana Mazembe itacheza na nani katika fainali kutokana na Bizertin na CS Sfaxien zote za Tunisia kutoka tena sare ya bila kufungana leo na sasa zitarudiana tena kesho.
Mfungaji wa bao la Mazembe leo, Tressor Mputu katikati akiwa na Ulimwengu kulia na Samatta kushoto

Katika mchezo wa kwanza, Mazembe iliifunga Malien mabao 2-1 mjini Bamako.

0 comments:

Post a Comment