"Nimekutana na kijana asub leo wakati natoka mazoezini akaniuliza;
"Kaka Nape mambo vipi? Mie mshabiki
kufa wa Chadema lakini sijapata mtu wa kunijibu kwanini Chadema kila
wakipanga maandamano wanapanga, Dar,Mwanza, Arusha na nimesikia
wanakwenda Mbeya tar. 10. Kwanini hawapangi maandamano anakotoka muasisi
wa Chadema Mzee Mtei?!!!"
Nikainama chini nikamuuliza uchaguzi
ndani ya chama chenu lini?! Akastuka kidogo, akanambia hivi unatakiwa
kuwa mwaka huu kweli!?!! "Mhhh hilo nalo swali! Lakini hivi tukifanya
uchaguzi Chama chetu kitapona kweli?! Nadhani bora tusifanya uchaguzi
mpaka tutakapokamata dola"! Alisisitiza kijana.
Nikamjibu "BWANA YESU KRISTO ASIFIWE" Says Nape
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment