Tuesday, 29 October 2013

WANAJESHI WALIO IBA VITU WESTGATE WAKATI WANAPAMBANA NA MAGAIDI WAFUNGWA

Nairobi, Kenya. Wanajeshi wawili nchini Kenya wamefutwa kazi na kufungwa jela kwa kitendo cha kupora mali wakati wa shambulizi la kigaidi kwenye Jengo la Westgate mwezi jana.  Hayo yamesemwa na mkuu wa jeshi la Kenya, Julius Karangi.

Karangi amesema kuwa mwanajeshi wa tatu aliyeshukiwa kwa uporaji anachunguzwa.

Awali Karangi alikanusha kuwa wanajeshi walifanya uporaji kwenye jengo hilo licha ya picha za CCT kuonyesha wanajeshi wakibeba mifuko ya plastiki kutoka kwenye moja ya maduka makubwa yaliyokuwa ndani ya Jengo la Westgate.

TUKIO ZIMA: WANANCHI WAJITOKEZA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU BALOZI ISAAC ABRAHAM SEPETU(BABA MZAZI WA WEMA SEPETU) NYUMBANI KWAKE SINZA

Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu enzi za uhai wake
Mh. Jaji Warioba  akisaini kitabu cha Maombolezo leo mchana nyumbani kwa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu jijini Dar es Salaam  
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe akisaini kitabu cha maombolezo leo October 29, 2013 nyumbani kwa marehemu Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu
Mama Gertrude Mongella akisaini kitabu cha maombolezo kwenye msiba wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu nyumbani kwake Sinza Mori leo October 29, 2013



 
Mh. Jaji Warioba na  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernard Membe wakibadilishana mawazo kwenye msiba wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu leo October 29,2013

Baadhi ya viongozi waliofika msibani kwa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu
Watu wa karibu na marehemu waliokuwa wanaishi naye huko Zanzibar wakizungumza jambo kwenye msiba wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu leo nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam
Mtoto mkubwa wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu, Aman Isaac Sepetu akizungumza jambo na mwandishi wa habari,  Mkwaiawa Kuhenga  leo October 29, 2013 nyumbani kwa Marehemu
Mtoto wa marehemu akimsalimia mama baada ya kufika msibani hapo leo mchana
Mama akiwa na mwanae baada ya kufika msibani
Wema Sepetu  (katikati) akiongea na Dada yake (wa kwanza Kushoto) na (kulia) ni mama yake mama yake mzazi

Sunday, 27 October 2013

DAVID BECKAM APATA AJALI YA GARI...SHUHUDIA PICHA HAPAAA

Collision: David Beckham reportedly crashes into another car has he pulls out of the driveway of his LA home

David Beckham reportedly crashed into another car as he pulled out of his Beverly Hills home.
The ex-England football captain was allegedly in his black Range Rover Sport with what looked like his son Brooklyn, 14, in the front passenger seat when the collision reportedly occurred at 2.30pm on Friday.

Onlookers say David, 38, pulled out of his driveway and hit an oncoming car being driven by a woman.

Collision: David Beckham reportedly crashes into another car has he pulls out of the driveway of his LA home
He reportedly reversed back into his drive way and waited within his residence

Mwanamke akamatwa na Polisi kwa kuuza bikira za watoto wake wa kike 12 kwa US$100 kila moja uko Colombia.

A woman and mother of 14 in Colombia tried to make ends meet by selling their daughters virginity for a couple hundred dollars.

Margarita de Jesus Zapata Moreno, colombian, 45, was arrested this week together with a 51-year-old contractor who police believe impregnated one of the young daughters.

She broke down in tears when she stood in front of the cameras after being arrested in Bogota, the Colombian capital. The Bogota Metropolitan Police say Zapata sold the virginity of 12 daughters to much older men seeking to have sex with young virgins.



Authorities also say the suspect would begin selling her daughters to men as soon as the girls
turned 12 years old. She charged anywhere between 300,000 and 400,000 Colombian Pesos ($160 to $212) for a virgin.

But Zapata strongly denies the accusation. Colombian authorities often show high-profile suspects to the media shortly after arresting them. When Zapata was standing in front of the cameras Wednesday, one of the reporters shouted a question to her: "Did you prostitute your daughters?" She answered: "No, my darling."

MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA ARUSHA(SAMSON MWIGAMBA) ASHUSHIWA KIPIGO CHA MBWA MWIZI NA VIONGOZI WENZAKE KISHA KUSIMAMISHWA KWA MUDA USIOJULIKANA...


Mkutano wa Baraza la Uongozi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini juzi uligeuka ukumbi wa ngumi, baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba kushushiwa kipigo.

Mwigamba alishushiwa kipigo hicho na baadhi ya viongozi wenzake wa chama kwa madai ya usaliti na tayari amesimamishwa uongozi kwa muda usiojulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas jana alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na viongozi hao wa Chadema kufikishana polisi.

Alikutwa na zahama hiyo mbele ya viongozi wakuu wa Chadema Taifa, Mwenyekiti, Freeman Mbowe na mwasisi wa chama hicho, Edwin Mtei katika Hoteli ya Coridal Spring.

Viongozi hao wamekuwa wakifanya ziara za aina hiyo nchi nzima, kuimarisha chama na kujipanga kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani na uchaguzi mkuu ujao wa Rais na wabunge mwaka 2015.

Habari kutoka ndani ya mkutano huo zinaeleza kuwa hatua hiyo ilifuatia tuhuma kwamba Mwigamba alituma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Jamii Forums, unaodaiwa kukichafua chama hicho.

Tukio hilo la aina yake lilitokea wakati viongozi wote wa juu wa chama hicho, wakiongozwa na Mbowe walipokuwa wakijadili mustakabali wa chama hicho, mkutano ambao ulihudhuriwa na wabunge karibu wote wa Chadema wa kanda hiyo.

Hata hivyo, wakati mijadala ikiendelea baadhi ya viongozi wa chama hicho, akiwamo Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema walimtuhumu Mwigamba kutuma ujumbe kwenye mtandao huo, uliokuwa ukizungumzia ufisadi ndani ya chama hicho, wakidai alitaka Mwenyekiti Mbowe kukubali kuchunguzwa.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Mwigamba alisema kuwa baada ya Lema kutoa tuhuma hizo aliungwa mkono na viongozi wengine na vijana waliokuwa wameimarisha ulinzi, kumvamia na kuanza kumpiga pamoja na kumnyang’anya kwa nguvu kompyuta mpakato (Laptop), aliyokuwa nayo, kisha kumpeleka Kituo Kikuu cha Polisi, mjini Arusha.

“Wamenipiga sana na kuniweka ndani, ila nashukuru Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Arusha (OCCID), alikuja na kunitoa saa 5:00 asubuhi,” alisema Mwigamba.

Alisema kuwa leo katika mkutano wake na waandishi wa habari ataeleza yote yaliyotokea na hatua atakazochukua, kwa kuwa yeye ni kiongozi wa juu wa chama.

Hata hivyo, alieleza kwamba bado anashauriana na wanasheria wake kuona kama anaweza kuwachukulia hatua waliompinga.

Kauli ya polisi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema polisi wameona hakuna kosa la

Newzz,,,,Jamal Malinzi achaguliwa kuwa Rais mpya wa TFF

 
Jamal Malinzi kushoto akiwa na swahiba wake, Rutayuga. Ameshinda Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kura 72 kati ya 126 zilizopigwa. Wallace Karia ameshinda nafasi ya Makamu wa Rais dhidi ya Nassib Ramadhabi na Imani

Friday, 25 October 2013

HIVI NDIVYO MWANAMUZIKI NYOTA WA NYIMBI ZA DINI ALIVYO PONA KATIKA AJALI HII.



Gari likiwa limepinduka bondeni.

Mwimbaji anayetamba na wimbo wa "Zawadi gani nitamtolea BWANA" ambaye pia ni mtume akichunga kanisa jijini Dar es Salaam John Komanya amepata ajali mbaya juzi mchana maeneo karibu na daraja la Mto Wami akiwa njiani kuelekea mkoani Arusha kukutana na viongozi wanaohudumu na mwalimu Christopher Mwakasege, kwa ajili ya mkutano wa injili ambao utakuwa na lengo la kuombea taifa kwa siku nne mwezi Disemba.


Akizungumza na GK mtume Komanya amesema lengo lilikuwa ni kupeleka barua kwa viongozi hao ili wamfikishie mwalimu Mwakasege kwaajili ya mkutano huo. Amesema akiwa njiani katikati ya Msata na Wami na wakati huo hakuwa amefunga mkanda wa gari, ndipo akasikia sauti ya Roho Mtakatifu ikimwambia kwa upole afunge mkanda lakini akawa anapuuzia na kuanza kujiuliza kwanini, sauti ikarudia tena kwa upole ikimwambia afunge mkanda akiwa bado anajiuliza ndipo anasema akasikia sauti ya Mungu ikizungumza kwa haraka na ukali "John funga mkanda" ndipo akafunga mkanda.



Mtume Komanya amesema akiwa anateremka kuelekea wami akiwa katika mwendo wa 180 wakati akipita katika kona kulikuwa na malori matatu mbele yake kukawa na lori lingine likifuatiwa na mabasi matatu yakipandisha kutoka Arusha kuja Dar, kwa wakati huo aliona malaika saba ambapo walishuka mithili ya makomandoo washukavyo kutoka kwenye kamba ya helikopta, mmoja akiwa amekaa kwenye boneti mbele, mwingine kulia, kushoto na mwingine nyuma yake ambaye alimwambia Komanya afuate maelekezo yake, anasema akiwa anamwangalia malaika aliyekaa karibu naye katika kiti cha dereva aliambiwa afuate maelekezo anayopewa na malaika wa nyuma yake.



Alipokuwa akiangalia mbele akaona gari linayapita mengine kwa spidi hali iliyomfanya Komanya kutaka kuingia katikati ya magari mengine lakini malaika akamwambia afuate maelekezo yake na kuambiwa aachie uskani jambo ambalo alilipinga kwakuwa aliona kifo mbele yake na kutaka kuingia katikati ili kukwepa, lakini malaika akamwambia ukiingia katikati utakufa, wewe achia usukani kama ninavyokwambia kwakuwa wametumwa kumlinda, akawa bado anatafakari kutokana na kuliona korongo kubwa upande wake huku malaika wakimwambia asiguse kitu chochote ikiwemo kutokanyaga breki lakini bila kusikia akakanyaga na kusababisha gari kuyumba sana, malaika akamwambia tena aachie breki na kuweka mikono yake kifuani. Anasema alipoweka mikono kifuani aliona wakiligonga lori huku malaika akiwa ameshika usukani na kuonyonga sana huku yeye akisema alijikuta akiwekwa kwenye kitu kama chupa ya maji, na yeye kwa wakati huo kuona kama vile yupo ndani ya glasi ya maji, ila anaona kinachoendelea.


Kisha baada ya hapo, upande wake wa usukani ndio uliogongwa, mara baada ya malaika kuchezesha usukani kidogo ili kuepusha madhara zaidi, na kisha ile semi-trailler ikamtupia kwenye korongo na kubinuka mara tatu hewani kabla ya kutua chini kwa mara ya nne, ambapo gari ilikuwa juu chini, yaani matairi yakiwa yanatazama juu.


Baada ya hapo kilichofuata ni kuendelea kusikiliza malaika wasemacho, ambapo hapo alisikia sauti ikisema fungua mkanada utoke, na kwa wakati huo kulikuwa na moshi ullioanza kutoka kwenye gari - na hapo akapewa dakika 12 kuchukua baadhi ya vitu alivyokuwa navyo kwenye gari. Maajabu ya Mungu, hakuna kitu chochote kilichogusa mwili wake, na wala hakuna damu iliyovuja kutokana na gari hilo kupindukia kwenye korongo.


Hakika utukufu ulimrudia Mungu kwa wakati huo kwani baadhi ya mashuhuda walikiri hapohapo ya kwamba hakuna mtu anayeweza kusalimika kwenye ajali hiyo, bali ni lazima tu mkono wa Mungu umehusika hapo kuokoa.


Baadhi ya mashuhuda ambao walikuwapo kwenye mabasi ya mkoa (hadi mkoa) walimtambua mtumishi wa Mungu ya kwamba ni John Komanya na hatumaye kumshukuru Mungu hapohapo, ambapo baadae Polisi walifika kwa ajili ya kazi yao - lakini hilo halikumzuia Mchungaji Komanya kupiga magoti na kumshukuru Mungu licha ya umati wa watu - na tukio hilo liliambatana na yeye kuisikia sauti ya Mungu ikimwambia "Nimekupa kazi ya kutengeneza kanisa langu,... usiogope nitakulinda, ila kuwa mwaminifu na nitakuweka kwenye uaminifu"


Sauti hiyo ilitoka kwa kiumbe ambacho kilikuwa na muonekano wa malaika, Pastor Komanya anaieleza GK na kusema kuwa sauti yake ilikuwa ya tofauti, na mavazi yake yalikuwa ni meupe na kwamba alielezwa dhahiri kuwa hiyo semi trailer ilikuwa imetumwa kummaliza, lakini ndio maana malaika walitumwa kumlinda.


"Zawadi Gani" kama ambavyo alikuwa akiitwa akiwa hospitali ya Muhimbili, alifanyiwa vipimo na kuonekana ya kwamba hana shida yoyote. Na hili linadhihirika hata pale alipotoka kwenye gari lililopiinduka, kwa kuwa alitoa vifaa vyake na kuanza pia kupiga picha, picha ambazo kama mtu akiziona zote, hakika hawezi kuamini kama kuna kusalimika hapo.

Uhaba wa maji UDOM na athari zake...


Wanafunzi UDOM waendelea na kilio cha uhaba wa maji chuoni hapo
- Wabainisha maji kidogo yanayopatikana yana chumvi sana

HIVI NDO VITU ALIVYO NAVYO MWANAFUNZI WA SIKU HIZI KICHWANI MWAKE

Wednesday, 23 October 2013

MANCHESTER UNITED 1 REAL SOCIEDAD 0: GOLI LA KUJIFUNGA LA MCHEZAJI MARTINEZ WA SOCIEDAD

An own-goal from Inigo Martinez as early as the second minute was enough for Manchester United to see off Real Sociedad at Old Trafford and move top of Group A.
Martinez deflected the ball into his own net after just 69 seconds after Wayne Rooney's initial effort cannoned back off the far post.
United capitalised on Shakhtar's heavy defeat by Leverkusen as they finished the night top of Group A with seven points from their three games.
On the rise: Manchester United moved to the top of Group A with a win against Real Sociedad
On the rise: Manchester United moved to the top of Group A with a win against Real Sociedad
Mistake: Inigo Martinez's early own goal gave Manchester United a perfect start at Old Trafford

WATANZANIA 3 WATIWA MBARONI WAKIWA NJIANI KWENDA KUJIUNGA NA AL-SHABAAB NCHINI SOMALI


Baadhi ya wanamgambo wa kikundi cha Al-Shabaab.
Jeshi la Ulinzi la Kenya liliwatia mbaroni Watanzania watatu ndani ya Somalia wakiwashuku kuwa walikuwa njiani kwenda kujiunga na Al-Shabaab, gazeti la The Standard la Kenya liliripoti siku ya Jumapili (tarehe 20 Oktoba).
Ali Ramadhan mwenye umri wa miaka 22, Musa Daudi miaka 19 na Shabaan Bakiri Waziri miaka 21, walitiwa mbaroni baada ya kuingia Somalia kutoka Kenya na sasa wanahojiwa katika kituo cha polisi cha Kiunga.
Polisi walisema kwamba washukiwa hao walitokea Dar es Salaam, wakasafiri hadi mpaka wa Tanzania na Kenya huko Lungalung, baadaye wakaenda kwa gari hadi Mombasa, Malindi na Lamu kabla ya kuingia Somallia.

PESA ZA MAFISADI USWIZI ZITTO KABWE AGONGA MWAMBA, SOMA ALICHOKIPATA HAPA


Kilicho kua matumaini kwa Watanzania chawa giza totoro. Hii ni kutokana na jibu la Mh. Zitto Kabwe toka Geneva alikokwenda kufuatilia Mabilioni yaliyofichwa huko. Imeonekana kagonga mwamba tena wa jabali. Soma jibu alilowajibu Watanzania katika post yake fecebook.
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO

EAC yakumbwa na mgawanyiko


Serikali ya Tanzania imekosoa Muungano mpya wa hiari wa nchi za Kenya,Uganda na Rwanda ulioundwa hivi karibuni.
Serikali ya Tanzania imeuelezea kuwa unaenda kinyume na makubaliano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hii ni ishara ya hivi karibuni kuwepo kwa mgawanyiko katika nchi wanachama katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.Wakuu wa nchi za Kenya,Uganda na Rwanda walikutana hivi Karibuni nchini Uganda ambapo walikubaliana kuanzisha miradi ya pamoja ya kimaendeleo katika nchi zao hatua ambayo haijapokelewa vema na Serikali ya Tanzania
Hii si mara ya kwanza kuzuka tofauti katika Jumuiya hii ambayo imeundwa ikiwa ni mara ya pili baada ya ile ya awali kuvunjika mwaka 1977 ,wakati huo ikiwa na wanachama watatu tu yaani Tanzania,Kenya na Uganda.
Mgogoro huu wa sasa inaelezwa kuwa chanzo chake ni mkutano wa pande tatu uliofanyika mapema mwezi July mwaka huu nchini Uganda ambapo nchi za Kenya,Uganda na Rwanda zilikubaliana kuungana katika kufanya miradi ya kimaendeleo ya pamoja ndani ya nchi zao,muungano ambao unaonekana kuitenga Tanzania,huku Burundi hivi karibuni nayo ikijiunga na Muuungano huo na kuufanya kuwa wa nchi nne.

Monday, 21 October 2013

ZITTO AANZA KAZI ILIYOMPELEKA USWIS


Habari zilizoenea  ni kwamba Zitto Amekwenda Uswiss kufuatilia mabilion ya yaliyotunzwa huko na mafisadi ...Jioni hii amepost kwenye facebook yake picha hiyo hapo juu akiwa na caption hii hapa chini:



"Siku ya kwanza ya kazi hapa Uswiss, mikutano mizuri sana na Waziri wa Fedha na timu yake, Shirika la Maendeleo #SDC na asasi ya #AllianceSud " Zitto

WANANCHI WAZUIA MSAFARA WA RAIS KIKWETE KWA MABANGO

Msafara wa JK ukiwa umezuiwa eneo la Mbwila Ludewa leo



 Wananchi  wa Mlangali  wakiwa  wamezuia  msafara wa Rais Kikwete
 Madai  ya  wana Ludewa kwa JK

Msafara  wa JK  ukiwa  umezuiwa  eneo la Mbwila Ludewa

WATANZANIA 11 WALIOKAMATWA WAKIFANYA MAFUNZO YA KIVITA YA AL QAEDA NA AL SABAAB HUKO MTWARA..!!




Hawa  ni  vijana  wa  kitanzania 11  ambao  walikamatwa  na  jeshi la polisi   Mtwara baada ya  kupata taarifa kwamba  walikua wakifanya mazoezi ya kivita kwa kutumia CD za  Al Qaeda na Al Shabaab ambapo walikamatwa na hizo CD  pamoja  na  silaha   mbalimbali  kama  ushahidi...

Taarifa ya jeshi la Polisi leo  imesema kuwa , vijana  hawa walipelekwa Mahakamani na watarudishwa tena tarehe 4 November 2013.
 

HATARIIII RELI YA TAZARA YAZIDI KUHUJUMIWA NAWAUZA VYUMA CHAKAVU MKOANI MBEYA

WAKATI SERIKALI IKIWEKA MIKAKATI YA KUNUNUA VICHWA VYA TRENI  YA TAZARA HUKU WENGINE WANAFANYA KAZI YA KULIHUJUMU SHIRIKA HILO KWA KUFUNGUA NA KUIBA MATALUMA YA RELI HIYO KUPELEKA KUUZA KAMA VYUMA CHAKAVU


HII HATARI SANA HAPA TAYARI WAMEFUNGUA NATI ZOTE

Saturday, 19 October 2013

AKINA SAMATTTA, ULIMWENGU NA MAZEMBE WATINGA FAINALI AFRIKA

BAO pekee la Tressor Mputu dakika ya saba, limeipa ushindi wa 1-0 Tout Puissant Mazembe dhidi ya Stade Malien ya Mali katika Nusu Fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi leo.
Matokeo hayo yanaifanya Mazembe yenye washambuliaji wawili Watanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu itinge fainali ya michuano hiyo.
Hata hivyo, bado haijajulikana Mazembe itacheza na nani katika fainali kutokana na Bizertin na CS Sfaxien zote za Tunisia kutoka tena sare ya bila kufungana leo na sasa zitarudiana tena kesho.
Mfungaji wa bao la Mazembe leo, Tressor Mputu katikati akiwa na Ulimwengu kulia na Samatta kushoto

Katika mchezo wa kwanza, Mazembe iliifunga Malien mabao 2-1 mjini Bamako.

"NIPO TAYARI KUNYONGWA KWAAJILI YA HILI ILA SITATOA RUZUKU KWA CHADEMA WALA CCM WASIPOKAGULIWA"...ZITTO


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Zitto Kabwe akitoa ufafanuzi juu ya taarifa yake ya mahesabu ya vyama 9 vya siasa ambavyo havijapeleka ripoti ya ukaguzi wake wa mahesabu kwa Msajili. Baadhi a vyama hivyo vilikanisha taarifa hiyo

KANISA LAGOMA KUMZIKA MUME WA UFOO SARO....LADAI KIFO CHAKE KINA UTATA..!!


Familia ya Anthery Mushi, aliyejiua kwa kujipiga risasi Jumapili iliyopita baada ya kumuua kwa risasi mkwewe, Anastazia Saro, amezikwa bila huduma ya kikanisa kijijini kwao Ongoma.
 

Kanisa Katoliki, Parokia ya Uru ilishindwa kutoa huduma hiyo kutokana na mazingira ya kifo chake.
 

Licha ya hali hiyo kujitokeza, familia hiyo, ilionyesha nia yake ya kwenda kumuangukia Paroko wa Parokia wa Kanisa hilo, ili aridhie familia ya Anthery, isome misa maalumu ya kuomba ndugu yao afutiwe dhambi inayomkabili.
 

Mushi (40), alijipiga risasi baada ya kumuua mkwewe na kumjeruhi mzazi mwenziwe Ufoo Saro, mtanzangazi wa kituo cha televisheni cha ITV,  eneo la Kibamba CCM, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
 

Wakati familia ya Mushi ikiazimia hilo, kiongozi aliyeteuliwa na familia kufanya ibada ya maziko, baba mdogo wa Mushi, Ugolin Mushi alisema kuwa Watanzania wanapaswa kutomhukumu kwa alichokitenda na kwamba imetosha kwa kuwa kinachoelezwa kila kona ya nchi baada ya tukio hilo ni sawa na mbu kubadilika na kuwa tembo.

VITUKO VYA ZITTO-AHUTUBIA WANANCHI KWA KUPITIA SIMU YA MKONONI


MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), juzi aliibua kituko baada ya kuwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara kwa njia ya simu. Zitto alilazimika kutumia njia hiyo katika Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora akiwa jijini Dar es Salaam, ili kuwanusuru viongozi wa chama chake waliokuwa katika ziara mkoani hapa wasipigwe na wananchi.

Viongozi walionusurika kupigwa na wananchi ni Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi wa chama hicho, Msafiri Mtemelwa aliyekuwa ameandamana na wenyeviti wa chama hicho wa mikoa ya Tabora, Katavi, Kigoma na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Magharibi, Shaaban Mambo.

Dalili za viongozi hao kuwa katika wakati mgumu, zilianza kuonekana mapema katika Kijiji cha Ibambo ambapo wananchi hao walishangazwa na hatua ya Zitto kutokuwapo katika msafara huo.

Matangazo ya awali ya mkutano wa chama hicho, yaliwatangazia wananchi uwepo wa Zitto katika mkutano huo, lakini mbunge huyo hakuonekana jambo ambalo liliwafanya wananchi kutoelewa.

Friday, 18 October 2013

NDUGU WA MCHUMBA WA UFOO SARO WASEMA NDUGU YAO HAKUJIUA.......................JE, KIBAO KITAMGEUKIA UFOO SARO AU?


Imeandikwa na JESSICA KILEO, Gazeti la Uhuru 

FAMILIA ya aliyekuwa mzazi mwenzake, Mwandishi wa ITV na Radio One, Ufoo Saro, Anthery Mushi (40), imevunja ukimya na kudai inapata wakati mgumu kuamini kwamba ndugu yao alijiua mwenyewe. Imesema suala hilo inaliachia Jeshi la Polisi lishughulikie ili kubaini undani wake.

Kaka wa marehemu, Isaya Mushi alidai hayo jana alipozungumza n,a waandishi wa habari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wakati mwili wa Mushi, aliyejiua kwa kujipiga risasi na kumuua mama mkwe wake, Anastazia Saro pamoja na kumjeruhi mchumba wake Ufoo, ukiagwa.

Mushi alidai wapo katika wakati mgumu wa kuamini kwamba ndugu yao alijiua mwenyewe, kwani haiwezekani mtu akajipiga risasi sehemu mbili ambazo ni kidevuni na upande wa bega la kushoto.

Alidai sio kazi yao kutoa hukumu, kwani wanasubiri upelelezi wa polisi kutoa jibu lililo sahihi kuhusiana na tukio hilo.

"Baada ya kifo cha ndugu yetu, wanafamilia tulifanya uchunguzi wa awali na bado linatuwia vigumu kutambua upi ni ukweli kuhusu jambo hilo kuhusiana na kifo hiki," alidai.

Zitto awakomalia CCM, Chadema


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali Zitto Kabwe akisisitiza jambo wakati wajumbe wa kamati hiyo walipofanya kikao na watendaji wa Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Katibu wa kamati hiyo, Michael Kadebe. Picha na Michael Jamson  


Dar es Salaam. Wakati Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe akisisitiza kuwa hesabu za Chadema ni miongoni mwa ambazo hazijakaguliwa, chama hicho kimeishutumu kamati hiyo kwa kuagiza kusitishwa kwa ruzuku kwa vyama vya siasa na kusema hatua hiyo ni ubabe.
Wakati Chadema wakitoa kauli hiyo, jana Zitto alisema vyama vya siasa tisa vikiwamo Chadema, CCM na CUF vinatakiwa kufika mbele ya PAC Oktoba 25 mwaka huu, kwa ajili ya kujieleza na kwamba chama kitakachokaidi, sheria za Bunge zinaeleza wazi, kwamba wahusika wanaweza kufungwa jela siku saba.
Chadema kilisema kuwa PAC kabla ya kuchukua hatua, ilipaswa kuwapa nafasi ya kuwasikiliza viongozi wa vyama husika, kumhoji Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Msajili wa vyama vya Siasa ambao wameshindwa kutimiza wajibu wa kukagua hesabu hizo kwa miaka minne.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chadema, Anthony Komu alisema jana kuwa, uamuzi wa PAC utaviathiri vyama kwani bajeti zake zimezingatia kuwapo kwa ruzuku.

Wednesday, 16 October 2013

MAJINA SITA YA WATANZANIA WALIOHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA...

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora, Simon Lukelelwa.

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora imewahukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa washitakiwa sita, baada ya kupatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia. Imetoa adhabu hiyo katika kikao chake kinachoendelea mkoani Shinyanga.

Adhabu hiyo ilitolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora, Simon Lukelelwa katika kesi nne tofauti. Kesi hizo ni za mauaji ya kikatili dhidi ya wanawake vikongwe, kutokana na imani potofu za kishirikina.

Mauaji hayo yalifanyika kati ya mwaka 2005 na 2007 katika Wilaya za Bukombe, Shinyanga na Kahama, ambako wanawake wanne waliuawa kikatili kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimbali za miili.

Waliopewa adhabu hiyo ni Venance Nuba na Tegemeo Paulo, ambao walitiwa hatiani kwa kosa la kumuua kwa kukusudia Sophia Gundu Januari 25,2006 katika Kijiji cha Kazibizyo Wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita.

Wengine wawili waliokumbwa na adhabu ya kifo cha kunyongwa ni Joseph Lushika na Maziku Mpiga Chai baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa kukusudia Monica Bulemela Mei 5, 2005 katika Kijiji cha Lutembela Wilaya ya Bukombe.
 

HIKI NDIO KISIMA CHA KISIMA CHA AJABU MKOANI DODOMA



KISIMANI 1 f3a53
Koo mbili za Wanyazaga na Wambukwa mnyambwa wakiwa wamekusanyika kukizunguka kisima kinachosemekana kimejaa maajabu cha Bwibwi kilichopo Katika kijiji cha Iyumbu kilichopo pembezoni mwa Chuo kikuu cha Dodoma [UDOM] 
MAJI 1 fb354
Baadhi ya wananchi wakifurahia kutumia maji yanayopatikana kisima cha Bwibwi kilichopo katika kijiji cha iyumbu Manispaa ya Dodoma, kisima hicho kilichovumbuliwa katikati ya miaka 1,800 kiko katika hatihati ya kufukiwa na eneo hilo lituumike kwa matumizi mengine.

Yathibitishwa, Dr Ndalichako OUT NECTA


Uthibitisho huu umetoka kwa mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Brof Rwekaza Mukandala kuwa Katibu Mtendaji wa NECTA Dr Joyce Ndalichako ameondoka NECTA na nafasi yake sasa inakaimiwa na Dr Charles Msonde aliyekuwa msaidizi wake.

MBUNGE MBARONI KWA WIZI WA GARI

Makalla anamtuhumu Ngonyani a.k.a Profesa Maji Marefu kuwa alichukua gari lake aina ya BMW X5 kisha akatokomea nalo kisha akawa anampigia simu hapokei na hata akimtumia SMS hajibu.
Kutokana na malalamiko hayo, hivi sasa Maji Marefu anasakwa na polisi wa Kituo cha Kati (Central), Dar es Salaam, tuhuma zikiwa ni wizi wa kuaminiwa, shauri lipo kwenye kitabu cha ripoti za polisi (Report Book ‘RB’) kwa namba CD/RB/13336/2013.
NYEUPE NA NYEUSI YA TUHUMA ZENYEWE
Nyeupe na nyeusi (black and white) ya tuhuma hizo, inawekwa wazi na ‘sosi’ wetu ambaye aliliibia siri kwamba sakata kati ya Maji Marefu na Makalla lilianza tangu Julai, mwaka huu wakati waheshimiwa hao walipokuwa ndani ya Jiji la Dar es Salaam.

“Maji Marefu aliomba gari la Makalla ili alitumie kwa mizunguko ya siku moja tu lakini hakurudisha,” kilisema chanzo chetu. “Mgogoro mkubwa ulianza kuibuka kuanzia hapo na mpaka leo waheshimiwa hao hawazungumzi kwa salamu wala kutakiana heri.”
Chanzo chetu kiliendelea kusema: “Siku ya kwanza tu ilipopita, Makalla alimpigia simu Maji Marefu akawa hapokei, akimtumia SMS hajibu. Kwa kifupi Makalla alipoteza mawasiliano na Maji Marefu lakini aliendelea kusubiri kwa sababu anajua ni mtu wake.”
Habari zaidi zinasema kuwa kilipita kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja bila ya Makalla kumpata Maji Marefu kwenye simu lakini walikutana katika Mkutano wa 12 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioketi kati ya Agosti 27 hadi Septemba 13, mwaka huu, Dodoma.

SHEKH SHARIF ALIYEPATA AJALI HALI YAKE YABADILIKA GHAFRA, WATANZANIA WATAKIWA KUMUOMBEA DUA APONE HARAKA!


Kijana shekh sharif Khamis “16” ambae amekuwa kwenye kalama kubwa za mwenyezi mungu kwa dua zake katika ya wiki hii amenusika kifo baada gari yake kupata ajali mbaya kupelekea kuzunguka zaidi ya mara tatu na hali yake sio nzuri kutokana na kuumia nyonga ya mguu wa kushoto.
Akiongea kwa shida kwa njia ya simu namba 0717-688792 Shekh sharif alisema kuwa ajali hiyo iliwapata wakati wakitokea kijiji cha Mwailanje kuelekea Kiteto Mkoani Arusha na wakiwa wanaelekea kwenye majukumu ya kiimani huku gari hiyo ikiendeshwa na ustaadh Seif Othman na bila kutarajia alitokea mtoto akiwa anaendesha baiskeli kwa kasi mbele yao na dereva alipoona mtoto huyo anakaribia kuivaa gari kwa mbele ndipo alipomkwepa.