Makamu
Mwenyekiti wa Yanga SC, Clement Sanga amesema kwamba uamuzi huo
ulifikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji jana mjini Dar es Salaam.
Sanga
amewaambia Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar
es Salaam kwamba Naggi ameajiriwa katika uongozi wa Yanga pamoja na Beno
Salvatory Njovu (Mshauri wa Mambo ya Utawala na Fedha) na George Simba
Magani atakayefanya shughuli za masoko.
Sanga
amesema kwamba waajiriwa wote hao wapya, nafasi zao rasmi zitatangazwa
baada ya miezi miwili, wakati Mwalusako anaendelea kukaimu Ukatibu,
wakati mchakato wa ajira rasmi ya nafasi yake unaendelea.
Kwa Hisani ya Bin Zubeiry
0 comments:
Post a Comment