Angalia Picha za Mwandishi wa The Citizen ajeruhiwa kwa Mapanga mkoani Singida
Mwandishi
wa habari wa gazeti la The Citizen na mwananchi mkoani Singida, Awila
Silla amenusurika kuuawa na mtu anadhaniwa kuwa Jambazi baada ya kukatwa
katwa kichwani na kusababisha kuzirai. Tukio hilo limetokea juzi saa
mbili usiku jirani na mahakama ya mwanzo ya Utemini mjini Singida. Awila
ambaye amelazwa wodi 2 hospitali ya mkoa amedai baada ya kukutana na
kijana huyo aliamuriwa kutoa Fedha na baada ya kudai hana, jibu hilo
lilisababisha kijana huyo kuanza kumkata Mapanga na alipoangauka na
kuzirai alinyang’anywa simu yake ya kiganjani .Hata hivyo Awila amedai
kuwa bado hajatoa taarifa ya tukio hilo polisi
0 comments:
Post a Comment