Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Rais wa
Kenya Uhuru Kenyatta amewahakikishia wakenya kuwa uongozi wa serikali
yake utaendelea kuwahudumia wakenya, licha ya kesi zinazomkabili yeye na
naibu rais William Ruto katika mahakama ya ICC jijini Hague huko
Uholanzi, ambapo pia mwanahabari Joshua Arap Sang anakabiliwa na baadhi
ya mashtaka kuhusiana na ghasia zilizoibuka baada ya uchaguzi wa mwaka
2007.
Rai
Kenyatta amewataka wakenya kutotiwa hofu na maneno ya watu wanaotaka
kutumia nafasi hiyo kueneza uvumi kuwa Kenya haitakuwa na uongozi ikiwa
rais Kenyatta na naibu wake watakapo elekea huko Hague badala yake
amewaambia kuwa wao hawana hatia na anaamini watashinda na ushindi huo
utakuwa wa wakenya.
Wakati
hayo yakijiri jijini Nairobi huko Mombasa mdahalo kuhusu hatua ya
wabunge wa Kenya kupitisha hoja ya kutaka taifa hilo kujitoa katika
mkataba wa Roma uliobuni mahakama ya kimataifa ya ICC, bado unaendelea
kupingwa na wananchi wakiwemo viongozi mbali wa kisiasa nchini humo.
Makamu wa
zamani wa rais Kalonzo Musyoka amesema kuwa suala la kujiondoa katika
mkataba wa Roma unaitangaza vibaya nchi hiyo kimataifa.
Rais
Kenyata na Naibu wake William Ruto wamepangiwa kuhudhuria baadhi ya
vikao vya kesi zao kwa pamoja baadaye mwezi huu ambapo naibu Ruto
anatarajia kuondoka nchini Kenya Jumatatu juma lijalo kuelekea Hague
Uholanzi ambapo rais Kenyatta atafuata baadaye.
0 comments:
Post a Comment