Monday, 4 November 2013

Yanga ni nuksi kwa wachezaji Mtibwa

Mshambuliaji huyu ambaye alikuwa tegemeo Mtibwa Sugar kabla ya msimu wa 2010 kusajiliwa na Yanga na kuiwezesha kutwaa Kombe la Kagame mwaka 2011 na pia kuibuka mfungaji bora, baada ya hapo amepotea.  

YANGA imeonekana kuwa ni timu yenye nuksi kwa wachezaji wanaotoka Mtibwa Sugar kwani wote waliohamia hapo Jangwani wakitokea Manungu, kwa sasa wanasugua benchi.
Kwa misimu mitatu mfululizo sasa, Yanga imesajili wachezaji kutoka Mtibwa. Waliotua hapo ni Said Bahanuzi, Juma Abdul, Hussein Javu na Rajab Zahir.
Ingawa kipa, Deogratius Dida, naye aliwahi kuidakika Mtibwa Sugar siku za nyuma, lakini alisajiliwa Yanga akitokea Azam FC.  Abdul na Bahanuzi wako muda mrefu ndani ya timu hiyo ingawa hawapati namba kutokana na nafasi zao kuwa na wachezaji wengine ambao hawakamatiki. Zahir na Javu ambao walikuwa tegemeo wakiwa Mtibwa Sugar,  wamesajili Yanga msimu huu. Hata hivyo nao wamekosa namba za kudumu na mara nyingi huishia benchi.

VITA YA ZITTO NA LEMA YAFIKA PABAYA, SOMA HAPA MKASA MZIMA



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh5S9FoCeny02FUzudAaIPHO9Sp0KdnrYQd9VGCq22_FNj7wrcxnmDu8IWdJhnrnpZl2ZgBaDT-lZ-fgYS_YZsyAfmUY4AKKmpnpZDh-r5U5FO05njwMq68slHVCHT88FyhsjaNuzmBaxtT/s1600/lemaaa.jpg
Vita vya maneno kati ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe imefika pabaya.
Vita hiyo ya maneno iliyoanzishwa na Lema katika kikao cha wabunge wiki iliyopita kwamba Zitto anafanya unafiki kukataa posho, jana iliingia katika hatua nyingine baada ya mwakilishi huyo wa Arusha kumshushia tuhuma Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kwamba anakataa posho za vikao bungeni, lakini anapokea posho nyingi kutoka mashirika mbalimbali ya kijamii nchini.
Lema aliweka tuhuma hizo kwenye Mtandao wa Jamii Forum huku akisema kuwa, suala hilo halihitaji vikao vya chama kulijadili isipokuwa vyombo vya habari na hususani mitandao ya kijamii kwani hata Zitto hutumia mitandao hiyo.
Katika hoja yake, Lema alisema kuwa Zitto ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) anakataa posho ya Sh70,000 kwa kikao kimoja cha Bunge, lakini anapokea Sh700,000 mpaka Sh1,000,000 kwa kikao kimoja cha kamati yake na haswa vile vinavyoandaliwa na mifuko ya jamii.http://2.bp.blogspot.com/-x7z8PGmhNb0/UnNi7F6LzYI/AAAAAAAAn4M/9FzceN8Hkhw/s1600/1.jpg
Hata hivyo, zitto alikanusha shutuma hizo akimtaka Lema kutoa ushahidi kama kuna mjumbe yoyote wa kamati ya PAC anayepokea posho, huku akieleza kuwa hawezi kubishana na Mbunge huyo wa Arusha mjini kwani yeye Zitto ni kiongozi wake ndani ya Chadema.
“Naomba kutaja masilahi yangu katika hili, wabunge wa kawaida wakialikwa katika vikao hivyo huwa wanalipwa Sh500,000 kwa kikao kwa siku . Mimi nimewahi kuhudhuria vikao hivyo mara mbili na nikalipwa hivyo pamoja na chai na chakula cha mchana.” alisema Lema.
Lema alisema posho hizo za wabunge ni tofauti na zile za Mwenyekiti wa PAC kwani yeye pamoja na posho ya Sh700,000 mpaka Sh1,000,000 hupewa mafuta ya gari au tiketi ya ndege ya kumtoa alipo na kumrudisha na kukodiwa hoteli yenye hadhi ya nyota nne mpaka tano ambayo kwa siku gharama yake ni Dola za Marekani 100 mpaka 600 kwa siku .
Akijibu hoja hizo, Zitto alisema tangu siku nyingi alikwisha piga marufuku kwa PAC kupokea posho kutoka taasisi au mashirika yanayosimamiwa na kamati hiyo.
“Toka nimekuwa Mwenyekiti wa POAC (Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma) sio tu nilipiga marufuku posho bali pia niliwashitaki PCCB (Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa) wabunge wanaochukua posho kutoka kwa taasisi za Serikali,” alisema Zitto.
Alieleza baada ya hatua hiyo, wabunge walihojiwa na PCCB kuhusu jambo hilo mpaka aliyekuwa Spika wa Bunge wakati huo, Samuel Sitta alipoingilia kati na kuwatetea wabunge hao.

Friday, 1 November 2013

"POSHO SIO DHAMBI ILA POSHO NI DHAMBI PALE POSHO INAPOKOSA UTU".... LEMA


Nimetafakari sana niliposoma kwenye magazeti kuwa sisi wabunge tumeongezewa posho bila hata sisi kufahamu jambo hilo .
Na kila mtu ametoa maoni mbali mbali juu ya jambo hili , ni kweli ni msimamo wa chama chetu (Chadema) kupinga posho mbali mbali zisizokuwa na tija na tulikubaliana hivyo kwenye vikao vya Chama Chetu vya Wabunge na kupinga mfumo wa posho uliopo kwa sasa ni msingi sahihi wa Chama kuonyesha hisia na ubadhilifu mkubwa unaotokana na ulipwaji mbaya wa posho kama ambavyo imejitokeza mara nyingi na hata hivi karibuni tumeshuhudia madudu mengi kwenye ripoti ya kamati ndogo ya Bunge iliyomchunguza Jairo. Lakini suala hili haliwezi kuepukwa kabisa na Chama kinajua ila utaritibu wa ulipwaji posho kwa watumishi mbali mbali wa umma ni tatizo kubwa na kuna mapungufu mengi sana ndio maana kupinga posho haina maana tu ya kupinga kiwango cha pesa anachopokea Mbunge au mtumishi yeyote wa UMMA bali mfumo mzima wa sera ya posho ili uweze kuwa na tija na kupunguza mianya ya wizi katika mfumo huu ambao umekuwa ukitumika vibaya kuliibia Taifa.

Pengine sisi wabunge ni vyema tukatambua kwanini wananchi wanapiga kelele kuhusu posho nilishawahi kusema Bungeni wakati nachangia kwenye Wizara ya Ustawi wa Jamii kuwa mshahara wa Wabunge , posho mbali mbali za Wabunge pamoja na marupurupu mengine yanaonekana kuwa anasa pale watumishi wengine wa serikali kama Manesi ,Asikari Magereza,Polisi ,Makarani Mahakamani wanapolipwa chini ya shilingi laki mbili na nusu kwa mwezi na wakati huo huo wanasikia mwakilishi wao akipiga kelele Bungeni kuwa posho ya laki mbili kwa siku ni ndogo. Ndio maana nimesema “POSHO SIO DHAMBI ILA POSHO NI DHAMBI PALE POSHO INAPOKOSA UTU , Na hapa lazima kutokee ugomvi wa kimasilahi na mgogoro mkubwa kati ya mwakilishi na anaye wakilishwa.


Pengine masilahi anayopata Mbunge ni ya kawaida sana tena sana ila yanaonekana kuwa anasa pale ambapo yeye kama mwakilishi anapolipwa kiwango cha posho cha siku moja ambacho ni sawa na mshahara wa mpiga kura wake kwa siku thelasini. Mimi nafikiri namna peke ya wabunge kutetea masilahi yao bora kwanza ni kupigania masilahi ya wapiga kura wote Tanzania na tukifanya hivi kama Wabunge hakuna Mwananchi hatakayeshangaa kwanini Mbunge awe na masilahi bora kwani ubunge ni nafasi kubwa pia inayositahili heshima kubwa kwani ni uwakilishi katika jamii.

Ebu jiulize wananchi wanaposikia Wabunge wamepewa milioni tisini kununua magari na wakati huo huo serikali imenunua bajaji kuwa ndio magari ya kubeba wakinamama wajawazito yaani (Ambulance) ni wazi kabisa wabunge wataonekani ni watu katili na walioenda bungeni kwa masilahi binafsi japo kuwa ukweli unabaki kuwa Wabunge wanahitaji magari imara na mazuri. Lakini Wabunge kama watafikiri Bajaj ni sawa kuwa gari la wakinamama wajawazito na wao kuchukua milioni tisini kwa magari ya binafsi bila kupiga kelele na kukataa unyanyasaji huu kwa wakina mama na Wagojwa ,hivyo ni dhahiri kuwa ugomvi hapa katika posho na masilahi ya Wabunge utasababishwa na tofauti ya masilahi dhidi ya wale waliowachagua kuwatetea ,Hivyo namna pekee Mbunge anaweza kutetea masilahi yake bora bila kuingiliwa na na kubugudhiwa ni Mbunge kuanza kufikiria masilahi ya watu wengine ambao pia ni watumishi wa UMMA ambapo yeye ni mwakilishi wake .

Nafahamu kuwa pamoja na kupinga mfumo mzima wa utaritibu wa posho ulivyo sasa tafakari ya kweli ni kwamba masilahi ya watumishi wa UMMA bado ni madogo sana kwa hiyo Uzalendo wa kweli sio tu kupinga masilahi bora bali serikali iwajibike kikamilifu kudhibiti wizi na ufisadi unaotokana na utaritibu mbaya wa ulipwaji posho , kuongeza makusanyo katika kodi mbali mbali ,kutumia rasilimali za Nchi vizuri ili masilahi ya watu wote Nchi hii yaweze kuwa na tija kwa maisha ya Watanzania na watu wengi waweze kuishi maisha ya faraja na kutimiza malengo yao muhimu ya maisha

Ndio maana nimesema “POSHO SIO DHAMBI ILA POSHO NI DHAMBI PALE POSHO INAPOKOSA UTU.

Nitakuwa ni mtu mwenye mashaka sana kama nikiwaza kuwa masilahi duni na maisha ya kuishi chini ya kiwango ni Uzalendo , Sasa Wabunge mkitaka msipigwe mawe barabarani ,msitukanwe , msionekane ni wasaliti wa jamii aliyowachagua , Sasa huu ni wakati wakusema , Mshahara wa Polisi ,Magereza,JWTZ, Walimu, Makarani Mahakamani na hata sekta zote za Serikali na Binafsi masilahi ya mishahara yao yaongezwe kwa asilimia kama ambavyo mmjiongozea nyie kwenye posho zenu tena zinazohusu siku moja tu lakini wao wanaomba kwa mwezi lakini hawapati. Sasa pamoja na kupinga mfumo mzima wa sera ya posho kama ambavyo Mwenyekiti wetu wa Taifa alisisitiza na kuomba sera hii iangaliwe upya ili kupunguzia Taifa mzigo mkubwa na kuboresha viwango vya mishahara vya watumishi wa UMMA , ni vyema nikarudia kusema kuwa ““POSHO SIO DHAMBI ILA POSHO NI DHAMBI PALE POSHO INAPOKOSA UTU.
Ni kweli gharama za Maisha zimepanda lakini hazikupanda kwa Wabunge tu pia kwa Wananchi wote wanaoishi Tanzania , Hivyo tukiacha ubinafsi tukawajibika vizuri

YANGA SC YAPAA KILELENI LIGI, YAIPIGA JKT 4-0…NGASSA MBILI PEKE YAKE

Shujaa; Ngassa amefunga mabao mawili peke yake leo
 
YANGA SC imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo, unaifanya Yanga SC itimize pointi 25 baada ya kucheza mechi 12, ikizishusha Azam FC na Mbeya City ambazo zina pointi 23 kila moja. Lakini timu hizo zinaweza kurejea kileleni baada ya mechi za kesho zikishinda.  Usindi wa Yanga leo umetokana na mabao ya mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa dakika za tatu na 12. Ngassa alifunga bao la kwanza kwa shuti kali la umbali wa mita 20, baada ya kufanikiwa kuwatoka mabeki wawili wa JKT Ruvu, wakati bao la pili alifunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa kurushwa na beki Mbuyu Twite. Pamoja na kumaliza dakika 45 za kwanza wakiwa nyuma kwa 2-0, lakini JKT Ruvu ndiyo waliocheza soka ya kuvutia ya pasi za hapa na pale, huku Yanga wakitumia mashambulizi ya haraka kwa mabeki kupeleka mipira pembeni, ambako mawinga wanatia krosi washambuliaji wagombanie goli. Kipindi cha pili, Yanga SC waliendelea na staili yao kushambulia kutokea pembeni, huku JKT Ruvu wakionekana kuanza kupoteza mwelekeo na kutoa mwanya zaidi wa kushambuliwa.  Beki Oscar Joshua aliipatia Yanga bao la tatu dakika ya pili ya kipindi cha pili, akiunganisha kona maridadi iliyochongwa na kiungo Simon Msuva. Kona hiyo ilitokana na kazi nzuri ya kipa wa JKT Ruvu, Sadick Mecks aliyepangua shuti kali la kiungo wa Yanga, Frank Domayo.   Jerry Tegete alikamilisha karamu ya mabao ya Yanga SC dakika ya 88 kwa pasi ya Simon Msuva na kuwafanya mashabiki wa timu hiyo waimbe nyimbo za furaha kuwabeza wapinzani, Simba SC ambao jana walilazimishwa sare ya 1-1 na Kagera Sugar kwenye Uwanja huo.
 Yanga SC; 
Deo Munishi ‘Dida’, Mbuyu Twite/Ibrahim Job dk45, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan/Relianst Lusajo dk78, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva,

VIFO VYA ASAKARI CHACHU KWA TANZANIA MEMBE


Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akizungumzia ushiriki wa Tanzania katika operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa popote pale duniani.

Waziri Membe akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mahojiano na mwandishi Fredy Mwanjala (kushoto) na mpiga picha Bi. Fauzia Yusuph (kulia), wote wanatoka Kituo cha Televisheni cha Channel Ten.


Na TAGIE DAISY MWAKAWAGO 
Tanzania itaendelea kushiriki operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa popote pale duniani. 
Msimamo huo wa Tanzania uliwekwa wazi na Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika mahojiano maalum na Mwandishi Fredy Mwanjala wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, yaliyofanyika leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam.  
Katika mazungumzo yao yaliyolenga kutaka kufahamu msimamo wa Tanzania kufuatia vifo vya askari wake huko Darfur, Sudan na hivi karibuni huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo (DRC), Waziri Membe alisema moja ya sera ya mambo ya nje katika awamu ya nne na Mhe. Rais Kikwete ni ulinzi na amani. 
Hivyo, Tanzania itaendelea kushiriki katika operesheni hizo za kulinda amani ambazo zimeiletea Tanzania heshima kubwa katika medani ya kimataifa. 
Waziri Membe alisema inawezekana kuwa wanajeshi wa Tanzania wanalengwa na kundi la waasi la M23, kwa kuwa Tanzania ni mwiba mkali kwa kikundi hicho kutokana na umahiri wake unaofahamika vyema katika nchi za Maziwa Makuu. 
“Umwagikaji wa damu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo (DRC) ni chachu kwa Watanzania dhidi ya kikundi cha waasi cha M23,” alisema Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.   
Hivi karibuni mwezi Agosti, kikosi cha M23 kilishambuliwa na kuteketezwa kwa mujibu wa taarifa za kiitelijensia zilizoripotiwa na vyombo vya habari.  Lakini inasemekana kuwa kuna kundi lingine limezuka tena hivi karibuni kwa jina hilo hilo la M23 kama vile chem-chem ya maji, alieleza Waziri Membe. 
“Ni muhimu ieleweke kuwa Tanzania haitosita kamwe kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kupambana na hizi vita za nchi jirani zisizoisha,” alisema Waziri Membe.  Aliongeza na kusema kuwa Tanzania imekuwa kinara cha medali za kimataifa katika kutetea na kulinda amani na usalama wa nchi yetu. 
“Sisi ni taifa ambalo liko tayari kujitolea kupigana na kumwaga damu katika kutetea amani na kutatua migogoro ya majirani zetu,” alisema Waziri Membe.  Alieza kuwa Tanzania imeshiriki kwa namna moja au nyingine katika vita vya ukombozi wa amani barani Afrika katika nchi za Msumbiji, Afrika Kusini, Zimbabwe, Comoro, Uganda, Mashariki ya Kongo-DRC na nchi nyingine nyingi.  
Akizungumzia kupoteza maisha kwa askari wa Tanzania nchini Kongo-DRC, Waziri Membe amesema kuwa ni msiba mkubwa wa kitaifa na wa Umoja wa Mataifa.  Alieleza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea salamu za rambirambi kutoka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Ulaya (EU), Serikali ya Kongo, Serikali ya Angola, Serikali ya Afrika ya Kusini na nchi nyingine duniani. 
Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazounda Brigedi Maalum ya umoja wa mataifa

Tuesday, 29 October 2013

WANAJESHI WALIO IBA VITU WESTGATE WAKATI WANAPAMBANA NA MAGAIDI WAFUNGWA

Nairobi, Kenya. Wanajeshi wawili nchini Kenya wamefutwa kazi na kufungwa jela kwa kitendo cha kupora mali wakati wa shambulizi la kigaidi kwenye Jengo la Westgate mwezi jana.  Hayo yamesemwa na mkuu wa jeshi la Kenya, Julius Karangi.

Karangi amesema kuwa mwanajeshi wa tatu aliyeshukiwa kwa uporaji anachunguzwa.

Awali Karangi alikanusha kuwa wanajeshi walifanya uporaji kwenye jengo hilo licha ya picha za CCT kuonyesha wanajeshi wakibeba mifuko ya plastiki kutoka kwenye moja ya maduka makubwa yaliyokuwa ndani ya Jengo la Westgate.

TUKIO ZIMA: WANANCHI WAJITOKEZA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU BALOZI ISAAC ABRAHAM SEPETU(BABA MZAZI WA WEMA SEPETU) NYUMBANI KWAKE SINZA

Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu enzi za uhai wake
Mh. Jaji Warioba  akisaini kitabu cha Maombolezo leo mchana nyumbani kwa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu jijini Dar es Salaam  
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe akisaini kitabu cha maombolezo leo October 29, 2013 nyumbani kwa marehemu Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu
Mama Gertrude Mongella akisaini kitabu cha maombolezo kwenye msiba wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu nyumbani kwake Sinza Mori leo October 29, 2013



 
Mh. Jaji Warioba na  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernard Membe wakibadilishana mawazo kwenye msiba wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu leo October 29,2013

Baadhi ya viongozi waliofika msibani kwa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu
Watu wa karibu na marehemu waliokuwa wanaishi naye huko Zanzibar wakizungumza jambo kwenye msiba wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu leo nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam
Mtoto mkubwa wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu, Aman Isaac Sepetu akizungumza jambo na mwandishi wa habari,  Mkwaiawa Kuhenga  leo October 29, 2013 nyumbani kwa Marehemu
Mtoto wa marehemu akimsalimia mama baada ya kufika msibani hapo leo mchana
Mama akiwa na mwanae baada ya kufika msibani
Wema Sepetu  (katikati) akiongea na Dada yake (wa kwanza Kushoto) na (kulia) ni mama yake mama yake mzazi