Mshambuliaji huyu ambaye alikuwa tegemeo Mtibwa Sugar kabla ya msimu wa
2010 kusajiliwa na Yanga na kuiwezesha kutwaa Kombe la Kagame mwaka 2011
na pia kuibuka mfungaji bora, baada ya hapo amepotea.
YANGA imeonekana kuwa ni timu yenye nuksi kwa wachezaji
wanaotoka Mtibwa Sugar kwani wote waliohamia hapo Jangwani wakitokea
Manungu, kwa sasa wanasugua benchi.
Kwa misimu mitatu mfululizo sasa, Yanga imesajili
wachezaji kutoka Mtibwa. Waliotua hapo ni Said Bahanuzi, Juma Abdul,
Hussein Javu na Rajab Zahir.
Ingawa kipa, Deogratius Dida, naye aliwahi
kuidakika Mtibwa Sugar siku za nyuma, lakini alisajiliwa Yanga akitokea
Azam FC. Abdul na Bahanuzi wako muda mrefu ndani ya timu hiyo ingawa
hawapati namba kutokana na nafasi zao kuwa na wachezaji wengine ambao
hawakamatiki. Zahir na Javu ambao walikuwa tegemeo wakiwa Mtibwa Sugar,
wamesajili Yanga msimu huu. Hata hivyo nao wamekosa namba za kudumu na
mara nyingi huishia benchi.
Said Bahanuzi
Mshambuliaji huyu ambaye alikuwa tegemeo Mtibwa
Sugar kabla ya msimu wa 2010 kusajiliwa na Yanga na kuiwezesha kutwaa
Kombe la Kagame mwaka 2011 na pia kuibuka mfungaji bora, baada ya hapo
amepotea. Alianza kuishia kukaa benchi lakini siku hizi hata jezi havai
anaishia jukwaani.
“Mimi naamini nina kipaji na najua mpira, lakini
kuwa majeruhi mara kwa mara kumechangia kupoteza mwelekeo wa soka langu,
bado napambana na naamini ipo siku nitacheza tu na kurudi kama zamani,
hakuna mtu ambaye hapendi kuanza kikosi cha kwanza, ila uamuzi wote ya
nani acheze unabaki kwa kocha,” alisema Bahanuzi.
Juma Abdul
Beki wa kulia wa kutegemewa wa zamani ya Mtibwa.
Alitua Yanga mwaka 2011, lakini alicheza kidogo kikosi cha kwanza ndani
ya timu hiyo kabla ya kupotezwa na ujio wa Mbuyu Twite anayeishikilia
nafasi hiyo.
Beki huyo, ambaye anasifika kwa mipira ya krosi,
amekuwa akipata nafasi ndani ya timu wakati baadhi ya wachezaji wa
kikosi cha kwanza wakiwa majeruhi au wanapotumikia adhabu. Pia amekuwa
akisumbuliwa na tatizo la kuwa majeruhi mara kwa mara, hata sasa
anasumbuliwa na uvimbe kwenye vidole vya mguuni. “Uwezo wa kucheza
kikosi cha kwanza ninao, lakini timu ina wachezaji wengi na kila mmoja
anataka kucheza hivyo kocha ndio anaamua nani aanze kikosi cha kwanza na
nani aanzie benchi ila uwemo mimi ninao mkubwa tu,” anakiri.
Hussein Javu
Alipokuwa Mtibwa msimu uliopita aliyewazamisha
Yanga katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Mtibwa
ilishinda mabao 3-0 wakati yeye akifunga mawili.
Wengi walidhani angeanza kikosi cha kwanza kwa
kiwango alichokionyesha Mtibwa, lakini kwa ushindani wa namba kwenye
nafasi ya ushambuliaji uliopo Yanga, amejikuta benchi likiwa ndio anga
zake
0 comments:
Post a Comment