Saturday, 21 December 2013

MASKINI YANGAAAA WALOAAAA TAIFA WAPIGWA 3 KWA 1 NA SIMBA TAZAMA HAPA UJIONEE

 Wekundu wa Msimbazi simba ya jijini Dar es Salaam leo imefanikiwa kwa mara nyinge kuzima kidomo domo, mikogo na mbwe mbwe za kila namna za watani wao wa jadi Yanga kwa kuwafunga magoli 3-1 katika mchezo maalum wa NANI MTANI JEMBE mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hii leo.
 katika mchezo huo Magoli ya simba yaliwekwa kimiani na mshambuliaji wake mahiri mwenye kasi nyingi na mbinu lukuki za ufungaji Hamisi Tambwe ambaye alipachika magoli 2 huku bao la tatu likifungwa na mchezaji aliyesajiliwa dirisha dogo kutoka Mtibwa Awazi Juma huku goli la Yanga likifungwa na Emmanuel Okwi.
 Patashika ya kuwania mpira
Hali jukwaa la yanga ilikuwa si shwari sana...
Ngome hata iwaje ndio Simba walipita...
Simba wao ilikuwa shangwe tu.

TAARIFA RASMI YA DKT. REGINALD A. MENGI YENYE KUJIBU MAELEZO YA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA MUHONGO KUHUSU HODHI YA VITALU



Reginal Mengi.
Baada ya Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara ((TNBC) uliofanyika tarehe 16 Desemba 2013, chini ya uenyekiti wa Mhe. Rais, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, sikutegemea kwamba Mhe. Profesa Muhongo angeendeleza mashambulizi dhidi yangu kwa sababu katika mkutano huo ambao ulikuwa na mafanikio makubwa tulifikia maamuzi ya kudumisha ushirikiano kati ya Serikali na Sekta Binafsi, kitu ambacho
nimekuwa nikipigania. Hivyo basi, kauli ambazo Mhe. Profesa Muhongo amezitoa Bungeni tarehe 19 Desemba 2013, zimenishtua na kunisikitisha sana. Ningependa kuwaeleza Watanzania wenzangu yafuatayo.
Profesa Muhongo ni muongo
Imefika wakati wa Watanzania kubaini kwamba Mhe. Profesa Muhongo ni mtu mwenye hulka ya kusema uongo. Kwa mfano:


1.       Kwenye kongamano la tarehe 8 Desemba 2013, Mhe. Profesa Muhongo alisema kwamba moja ya kazi yake, alipokuwa akifanya kazi kama mwanasayansi huko nje, ilikuwa kutabiri umuhimu wa sayansi katika uchumi wa dunia miaka 3,000 ijayo. Huu ni uongo wa mchana kweupe.

2.       Mnamo Julai 2012 Mhe. Profesa Muhongo aliwaahidi Watanzania kwamba hakutakuwa na mgawo wa umeme tena. Sote tunashuhudia mgao wa umeme ukiendelea hadi sasa.

3.       Mnamo mwezi Septemba 2012, Mhe. Profesa Muhongo alinukuliwa akizungumzia mikataba ianayohusiana na vitalu vya gesi akisema kwamba “baadhi ya mikataba ni ya ovyo, na inahitaji kuvunjwa” na “sitovumilia mikataba ambayo haina maslahi kwa nchi na inawanufaisha wachache”. Baada ya hapo, Mhe. Profesa Muhongo aliamrisha Bodi mpya ya TPDC kusitisha ugawaji wa vitalu vya gesi uliopangwa kufanyika mwezi huo na kupitia upya mikataba yote iliyokuwepo awali. Sasa zaidi ya mwaka umepita na Mhe. Profesa Muhongo hajarekebisha mkataba hata mmoja.

Profesa Muhongo na takwimu zake za maeneo ya madini

1.       Tarehe 8 Desemba 2013, alipokuwa anajibu swali la Mhe. Tundu Lissu kuhusu ni nani anamiliki migodi ya Tanzania, Profesa Muhongo alitoa takwimu za kuonyesha kwamba mimi ninamiliki eneo kubwa mara tatu ya Dar es Salaam kupitia kampuni zangu tanzu.

2.       Jumapili iliyopita mimi nilimjibu Mhe. Profesa Muhongo kwa kumueleza kwamba takwimu zake kuhusu mimi ni za uongo, na vilevile hizo alizotoa Bungeni pia ni za uongo na nilimweleza kwamba swali la Mhe. Tundu Lissu lilikuwa ni “nani anamiliki maeneo ya migodi”.

3.       Katika eneo la kutafuta madini unaweza ukapata au ukakosa – ni bahati nasibu, ndiyo maana maeneo ya utafutaji yanakuwa makubwa. Vilevile wakati unatafuta madini shughuli nyingine za wananchi waliopo katika eneo hilo huwa zinaendelea, kwa mfano kilimo, makazi, uchimbaji mdogo mdogo nk. Unapopewa leseni ya mgodi inamaana kwamba tayari umeshapata bingo – madini yapo na unaanza kuchimba. Kwa mantiki hiyo maeneo ya migodi inakuwa midogo – isiyozidi kilomita 10 za mraba, na shughuli zote za wananchi katika eneo hilo zinasitishwa.

4.       Sasa kwenye maelezo yangu ya Jumapili iliyopita nilitamka wazi kwamba mimi ninamiliki kwa ubia na Watanzania wenzangu mgodi mmoja tu wa uchimbaji wa madini ya Tanzanite wenye eneo lisilofikia hata kilomita moja ya mraba. Profesa Muhongo hajakanusha hili, badala yake anaturudisha Watanzania kule kule kwenye maeneo ya utafutaji badala ya migodi.

5.       Siyo hilo tu.  Mhe. Profesa Muhongo anafahamu kwamba kuna aina 6 za leseni za utafutaji na uchimbaji wa madini. Lakini kwa makusudi kabisa Mhe. Profesa Muhongo anafananisha leseni ya Mtanzania anayetafuta au kuchimba kokoto na leseni ya mwekezaji wa kigeni anayetafuta au kuchimba urani au dhahabu. Kweli unaweza kufananisha kokoto na dhahabu?

6.       Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa utafutaji madini (mineral prospecting) ndiyo msingi wa maendeleo ya sekta ya madini kwa sababu bila utafutaji hakuna ugunduzi na uendelezaji wa migodi hapa nchini. Lakini kuanzia Julai mwaka jana Waziri  Muhongo alipandisha tozo za vitalu kwa asilimia kati ya 100 na 500. Matokeo yake Watanzania wengi wanarudisha leseni zao na kasi ya ugunduzi wa migodi imepungua.

HII HATARI ANG'ATWA SIKIO NA KUNG'OLEWA KABISA KISA KIKIDAIWA KUWA WIVU WA MAPENZI..!!

 
Hivi karibuni hapa jiji mwanza mkazi mmoja wa Igoma Aliefahamika kwa jina moja la Consolata amepigwa na mmewe na kung’atwa sikio na mtu anaedaiwa kuwa ni hawara wa mumewe bi consolata amesema alikuwa akigombana na mumewe ndipo hawara yake huyu alipokuja na kusema ngoja tukuonyeshe maana hutujui ndipo alipong’atwa sikio na kuondolewa sikio zima

Mara baada ya kufanyiwa ukatili huo alienda kulipoti katika kituo cha polisi lakini kwa madai yake ni kwamba watuhumiwa waliachiwa huru kwa kuwa walikuwa wakijuana na baadhi ya askari waliokuwepo kituoni .Ndipo bi consolata alipochukua hatua za kutafuta wasamalia wema kama waandishi ili waweze kumsaidia aweze kupatiwa matibabu kwani ni mgeni jiji mwanza toka kigoma na alikuja mwanza kwa ajili ya kumsalimu mumewe.

Baada ya kuzungumza na waandishi alipelekwa kwenye taasisi ya kivulini ambao mpaka sasa wanampatia huduma ya matibabu ukatili huu kiukweli ni aibu kubwa kwa taifa letu

Tuesday, 10 December 2013

Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Gabriel Kimolo ahamia CHADEMA



Gabriel Kimolo
Katika hali ya kuonyesha CCM hapako shwari leo mkuu wa Wilaya Gabriel Kimolo amevua gamba na kuvaa Gwanda hii leo ni kwenye Kongamano linaloendelea muda huu katika hotel ya Land mark ambapo wangeni rasmi ni Tundu Lisu, Mnyika, Lema, Msigwa, Heche na Kilewo.

Akiongea na watanzania waliojana kwenye kongamano hilo Kimolo amesema CCM inakufa na kuna kila ishara za CCM kufa mfano kuuwa waandishi wa habari, kutesa wana harakati, kutumia nguvu nyingi kuzoofisha upinza hasa CHADEMA pia amewaomba watanzania kujiunga na chadema kwani kwasasa ni tumaini la watanzania na kuna kila ishara kuwa inaenda kuongoza nchi...

HABARI KAMILI
Kwa mujibu wa Bw. Kimolo, miongoni mwa sababu za kujiuzulu kwake ni pamoja na kitendo cha yeye kukashifiwa na baadhi ya wafanyibiashara wanunuzi wa kahawa Wilayani hapo, ambao walifikia hatua ya kumtamkia kuwa hawawezi kuongea na "mbwa, bali na mfuga mbwa", wakimaanisha hawawezi kuongea naye bali Waziri Maghembe ambaye inadaiwa alikuwa akiwakumbatia.

HAWA NDO WEZI 5 BORA WA MTANDAONI (HACKERS)

TOP FIVE HACKERS of the world

 (1)Gary McKinnon:
USA declared him as the biggest military computer hacker ever. He hacked the security system of NASA and Pentagon. This made him one of the great black hat hacker celebrities and got his name into the hacker's community. The nerd is now facing 70
years of imprisonment and is deprived from accessing internet. He has illegally accessed 97 computers and has caused around $700,000 damage to the economy. ...

(2)Robert Tappan Morris:
He is the creator of first internet worm ?Morris worm? he was a student at Cornell and from that where he started writing codes to create worms as he wanted to know how large the internet world is. But the worm lead to the slow speed of internet and made the systems no longer usable. There was

no. ways to know how many computers were affected but the experts alleged that around 6000 machines. He was sent to 3 years imprisonment, 400 hours of community service and was fined $10,500. At present he is a professor at Massachusetts institute of technology, computer science and artificial intelligence laboratory. He was the first person
prosecuted under the 1986 Computer Fraud and Abuse Act.

(3)Kevin David Mitnick:
The computer security consultant, author and a hacker was accused of many cases. He broke into the computer of top technology and telecommunications like Nokia, Motorola, Fujitsu Siemens and sun Microsystems. He termed his
activity as social engineering? to legalize his acts. He hacked the Los Angeles bus transfer system to get free rides the biggest hacking was the breaking into the DEC system to view the VMS source code (open virtual memory system which lead to the clean-up cost of around $160,000. He also gained
the full administration privileges to IBM minicomputers at the computer learning institute in Los Angeles for a bet.

Jinsi mandela alivyofunika Dar, Zanzibar baada ya kutoka gerezani


Mwalimu Julius Nyerere akiwa na mgeni wake Nelson Mandela (kushoto) na Winnie Mandela kwenye gari la wazi wakati wakiwasili kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Mandela alifanya ziara nchini mwaka 1990 baada ya kutoka gerezani.Picha na Maktaba. Dar es Salaam. Siku 23 baada ya NelsonMandela kuachiwa huru kutoka gerezani,

Tuesday, 3 December 2013

JE WAJUA KUWA NGUCHIRO NDIYE MNYAMA BINGWA WA KUUA NYOKA NA ANAE MUOGOPA COBRA?


Nguchiro-Jangwa


Na Lwitiko Peter 
JE WAJUA?
Nguchiro bingwa wa kuua nyoka anayeogopa cobra

NGUCHIRO ni mnyama mdogo jamii ya panya, anayepatikana kwa wingi barani Afrika na kusini mwa mabara ya Ulaya na Asia.

Kuna kama jamii 33 hivi za nguchiro. Lakini kuna jamii nyingine nne za ziada ambazo hupatikana huko Madagascar.

 Hawa ni jamii ndogo ya Galidiinae. Awali, jamii hizi nne ziliwekwa katika kundi la wanyama wengine wanaopatikana huko Madagascar lakini baadaye ikaja kujulikana kuwa wana sifa tofauti, hivyo kuundiwa makundi yao yanayojitegemea.

Utafiti wa kijenetiki unaonyesha kuwa Galidiinae wana uhusiano wa karibu na wanyama wengine wa familia ya Eupleridae, ambao wanakaribiana sana na nguchiro.

Mwonekano

Kama tulivyodokeza hapo juu, nguchiro hupatikana kwa wingi katika maeneo ya Afrika na kusini mwa Ulaya na Asia. Lakini pia kwa kiasi kidogo hupatikana huko Puerto Rico na sehemu ya visiwa vya Caribbean na Hawaiian.

MADIWANI CCM,CHADEMA WAPIGANA NGUMI KAVUKAVU



Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya,Diwani Athuman

Madiwani wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya, wamejeruhiwa vibaya hadi kulazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa kile kinachodaiwa kupigwa na wenzao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika eneo la ukumbi wa halmashauri wa Mkapa wakati kikao.

Diwani wa Kata ya Mwakibete ambaye pia ni Katibu wa Mwenezi Chadema wilaya ya Mbeya Mjini, Lucas Mwampiki, jana aliwaeleza wandishi wa habari kuwa tukio hilo lilutokea Ijumaa iliyopita katika ukumbi wa Mkapa ambao unamilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Mwampiki aliwataja madiwani waliojeruhiwa na kulazwa kuwa ni wa Kata ya Sinde, Fanuel Kyanula na wa Kata ya Ilemi, Furaha Mwandalima.

Mwampiki alisema kabla ya kutokea kwa vurugu hizo, madiwani wa vyama vya upinzani walikuwa wakihoji uhalali wa ziara ya baadhi ya maofisa wa Halmashauri ya Jiji wakiongozwa na Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga, kwenda China kwa kutumia fedha za halmashauri bila kufuata utaratibu.

Alisema katika ziara hiyo, Meya Kapunga aiongozana na maofisa watano ambao ni Mkurugenzi wa Jiji, Mchumi, Afisa Mipango na diwani mmoja wa CCM ambayo iliigharimu halmashauri hiyo zaidi ya Sh. milioni 95 ambazo hazikuwa kwenye bajeti wala kuidhinishwa na kikao chochote.

Alisema madiwani wa Chadema na NCCR-Mageuzi walifuata taratibu zote za kuhoji suala hilo, ikiwa ni pamoja na kuorodhesha majina yao na kusaini ili mkutano wa madiwani uitishwe na hoja hiyo ijadiliwe.

Kwa mujibu wa Mwampiki, kikao cha Madiwani kilichoketi Ijumaa waliamini kuwa ajenda hiyo itaingizwa, lakini wakashangaa kuona haimo kwenye orodha ya ajenda zilizopaswa kujadiliwa.

Alisema madiwani wa upinzani walipohoji juu ya kuondolewa kwa ajenda hiyo, Meya Kapungu ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho, alikuja juu na kuamuru mlango ufungwe ili madiwani wapigane.

“Tulishangaa kusikia Meya akisema kuwa kila siku madiwani wa Chadema tunawafanya wasiishi kwa raha mjini na kutamka kuwa inabidi milango ifungwe ili zipigwe,” alisema Mwampiki.

Alisema madiwani wa Chadema kuona hivyo waliamua kutoka haraka nje ya ukumbi wa mkutano, huku wakirushiwa chupa za maji na baadhi ya madiwani wa CCM.

Mwampiki alidai kuwa hata baada ya madiwani wa Chadema kuwa wametoka nje ya ukumbi wa mkutano, madiwani wa CCM waliwafuata na kuanza kuwashambulia kwa kipigo mpaka walipoachanishwa na polisi waliokuwepo eneo hilo.

Alisema katika vurugu hizo, madiwani wawili wa Chadema walijeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa kwa matibabu na walilazwa.

Asema Diwani wa Ilemi, Mwandaliwa alijeruhiwa sehemu za shingo kiasi cha shingo yake kutogeuka kila upande huku Diwani wa Sinde, Fanuel akiwa amejeruhiwa kwenye shavu kutokana na ngumi walizokuwa wakipigwa.

Akizungumza baada ya kutoka hospitali, Mwandalima alisema alikuwa miongoni mwa madiwani wa mwisho kutoka ukumbini na kuwa alipofika nje ya ukumbi alijikuta akivamiwa na kundi la madiwani wa CCM ambao walianza kumshushia kipigo huku wengine wakimkaba na kumuumiza vibaya maeneo ya shingoni.

Meya wa Kapunga alikanusha kuhusika na ugomvi huo huku akisema kuwa hakuna diwani aliyepigana ndani ya ukumbi wa mkutano.

Alisema anachokumbuka ni kwamba madiwani wa upinzani walikuwa na hoja ya kutaka kujua juu ya ziara ya watumishi wa Halmashauri nchini China, lakini hawakufuata utaratibu na kanuni  walizojiwekea katika kuhoji masuala mbalimbali ya halmashauri.

Alisema baada ya kupitia orodha ya majina ya madiwani waliokuwa wakihoji suala hilo, walibaini kuwa kuna baadhi ya saini za madiwani zimeghushiwa, jambo ambalo alisema ni kinyume cha taratibu za halmashauri na sheria za nchi.

Alisema miongoni mwa saini zilizobainika kughushiwa ni za baaadhi ya madiwani ambao hawapo jijini Mbeya kwa muda mrefu.

Alisema baada ya hoja ya madiwani hao kukataliwa, ndipo walipoinuka kutoka ndani ya ukumbi wa mikutano huku wakiwatolea matusi ya nguoni madiwani wenzao wa CCM.

“Ninachokumbuka ni kwamba wakati madiwani wa Chadema wakitoka nje walikuwa wakitukana matusi ya nguoni inawezekana matusi hayo yaliwauma wenzao wa CCM ambao waliwafuata huko nje, hivyo kama walipigwa nje ya mkutano mimi sina taarifa,” alisema Kapunga.

Akizungumzia ziara ya watumishi wa halmashauri ya akiwamo yeye nchini China, Kapunga alisema ziara hiyo ilitokana na agizo la serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (Tamisemi).

Alisema kabla ya kufanya ziara hiyo alifuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kulijulisha Baraza la Mdiwani la Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Ofisi ya Katibu Tawala ya Mkoa wa Mbeya, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Mussa Zungiza, alipinga kiwango cha fedha cha Sh. milioni 95 kinachodaiwa na madiwani wa Chadema kuwa kilitumika kwenye ziara hiyo, badala yake alisema zilitumika Sh. milioni 54.

WAATHIRIKA WA UKIMWI WAGOMA KUTUMIA DAWA ZA ARV'S.



WAGONJWA 272,939 wameacha kutumia dawa za kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi (ARV’s). Kutokana na hali hiyo, virusi vya ugonjwa huo vimeanza kuwa sugu kwa kuwa havipati dawa za kupambana navyo. 
Taarifa hiyo ilitolewa na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Dar es Salaam.

Tafiti zinazoendelea kufanyika zimeonyesha kuwa, mtu anayetumia ARV’s inavyostahili uwezekano wa kumwambukiza mwenzake unapungua hivyo nawashauri watu waendelee kuzitumia, naomba wasiache kwa sababu sasa tunaambiwa theruthi moja ya walioandikishwa hawatumii ARVs, ”alisema Dk. Bilal.

Pia alizitaka mamlaka husika kuchukua hatua kali kwa watu wanaosambaza dawa bandia za ARV’s.

Kulingana na takwimu za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii hadi kufikia Juni mwaka huu watu milioni 1.2 walikuwa wamesajiliwa kwa ajili ya tiba na matunzo na kati yao waliokuwa wameanzishiwa ARV’s ni 736,664 lakini wanaotumia ni 463,725.

Uvivu wa Wabongo kupiga kura umemkosesha tuzo AY


Jumamosi ya November 30, tuzo za 10 za video za Channel O aka CHOAMVA zilitolewa huko Kliptown, Soweto (Johannesburg) nchini Afrika Kusini.
Mwaka huu ni AY pekee ndiye alikuwa msanii wa Tanzania aliyekuwa akiwania tuzo hizo. AY alikuwa akishindania kipengele cha video bora ya Afrika mashariki na video bora ya msanii wa kiume Afrika.
Bahati mbaya, AY hakufanikiwa kututoa kimasomaso na P-Unit kuchukua tuzo ya video bora ya Afrika Mashariki. Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa Twitter, utagundua kuwa AY alikuwa akipiga kampeni ya nguvu kuwaomba watanzania wampigie kura. Marafiki zake, wasanii wenzake na vyombo vya habari vilimsaidia pia kuufisha ujumbe huo bila kuchoka.
Kampeni ilikuwa kali kiasi cha kumtia yeye mwenyewe moyo kuwa huenda mwaka huu angeibuka na tuzo pia na kutupa sifa Tanzania. Hata hivyo mambo yalienda tofauti na AY hakufanikiwa kupata tuzo.
Lakini ukweli unaouma ni kwamba, wabongo tumekuwa ni watu wa kuongea bila vitendo. Hakuna ubishi kabisa kuwa Watanzania wengi waliokuwa na uwezo wa kumpigia kura hususan kwenye internet ambako ni bure, hawakufanya hivyo sembuse kwa sms ambako fedha hukatwa?
Tumekosa uzalendo na kupenda vya kwetu. Badala yake tumekuwa ni watu wa kupuuzana na kuchukuliana poa tukiwathamini watu wa nje kuliko wazawa.
P-Unit hawakuwa na nguvu kama aliyonayo AY lakini wamefanikiwa kuitwaa tuzo hiyo kwakuwa Kenya ilikuwa nyuma yao. Tujifunze kuwa nyuma ya wasanii wetu pale wanapokuwa wanahitaji kura zetu kwenye mashindano ya kimataifa kwakuwa bila support ya nyumbani hawawezi kufika popote.
Mpaka sasa AY bado hajasema chochote lakini swahiba wake walienda naye Afrika Kusini, Mwana FA alitoa shukrani kwa niaba yake.

KAMA ULIKUWA HUJUI KWAMBA TUI LA NAZI LINAUA VIRUSI NA MAFUTA YANANG’ARISHA NGOZI SASA CHEKI HAPA...!

 
KATIKA makala iliyopita tuliona jinsi mwili unavyoweza kujitibu wenyewe ukipata mlo sahihi. Leo tunapenda kuzungumzia faida za nazi, ambazo zinatokana na kuwa na mchanganyiko maalum wa aina nyingi za mafuta zijulikanazo kama ‘medium chain triglycerides’ au kwa kifupi (MCT’s).

 
Nazi ikiliwa na binadamu hugeuza aina hizo za mafuta kuwa tindikali ambayo kitaalamu huitwa ‘medium chain fatty acids’ au kwa kifupi (MCFA’s) ambazo huua na kutokomeza virusi vya aina mbalimbali mwilini.

Tui la nazi
Matumizi ya nazi kama tiba kwa waathirika wa virusi duniani yalilipuka kwa kasi mwaka 1990 mara baada ya mtafiti wa tiba kutoka Iceland, Bw. Halldor Thormar, kubaini maajabu ya tiba hii.

Waathirika wa virusi vya aina mbalimbali duniani waliotumia nazi walitoa ushuhuda wao wa namna walivyopata nafuu mara baada ya kutumia nazi kama tiba. Licha ya kuponya maradhi waliyokuwa nayo, iliwaboreshea afya zao na kuonekana kana kwamba si waathirika tena.

Monday, 2 December 2013

HIVI NDIVYO WAPENZI WA SIMBA WALIVYOMPOKEA KOCHA MPYA ALIYERITHI MIKOBA YA KIBADENI MTAA KLABU YA SIMBA SC.


Mashabiki wa Timu ya Simba, wakimpokea kwa shangwe na nderemo, kocha wao mpya aliyetua nchini jana machana. 


Mara kadhaa kumekuwa kukitokea furaha kwa mashabiki, viongoni na hata wachezaji wa Klabu zetu kubawa hapa nchini, wakati wanapokuwa wanamkaribisha Kocha mpya ama kumtambulisha kwa mbwembwe nyingi, lakini anapotokea kukosea kidogo haijalishi ni muda gani amekwisha kaa na Klabu husika, anaweza kutimulia ama kuanzishiwa mizengwe hadi akakata tamaa ya kuonyesha yale yote aliyojiandaa nayo kuifanyia Klabu husika.


Wakati umefika sasa kwa Klabu zetu kufunguka kifikra na kuwa na upeo wa kufikiri ili kuziendeleza klabu zetu, kwa kuwaachia makocha waweze kufanya yale yanayostahili bila kuingiliwa na viongozi ama watu flani kwa pesa zao ama umaarufu wao katika klabu. 


Huko nyuma walikwishapokelewa makocha kadhaa kama alivyofanyiwa kocha huyu leo na waliondoka kimya kimya huku wengine wakiondoka klabuni kwa mafalakano na viongozi wa klabu.

Kocha huyo akikabidhiwa taji la maua na mashabiki baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Dar leo.

Akipata menu.....

Kocha huyo akiongozana na baadhi ya viongozi wa Simba wakati alipotembelea na kukagua uwanja wa mazoezi wa Klabu hiyo wa Kinesi.Picha kwa Hisani ya Lenzi ya Michezo

BREAKING NEWS !!! BARABARA YAZIBWA ENEO LA MTO WAMI BAADA YA MALORI, ANGALIA PICHA HAPA



Malori yaliyogongana yakiwa yameziba njia baada ya kugongana eneo la mto wami.  Foleni ni kubwa sana ya mabasi yaendayo mikoa ya Tanga,Arusha Na Kilimanjaro.
Ajali mbaya imetokea muda huu eneo la mto Wami na kusababisha Foleni kubwa sana kwa magari na mabasi yanayotumia njia hiyo.
Chanzo cha ajali hiyo inadaiwa ni kufeli breki kwa malori hay o

DK SLAA, MBOWE WAPIGWA MARUFUKU KUKANYAGA ARDHI YA MWANZA




Mwanza, Tanzania. Gazeti la RAI leo katika ukurasa wake wa kwanza limeandika kwamba Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na  Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa amepigwa marufuku kukanyaga jijini Mwanza ambako chama hicho kimepanga kwenda kuwahutubia wananchi.

Mbali na kupigwa marufuku, viongozi wa Chadema wamepewa masharti ya kufanya kila linalowezekana kumrejesha madarakani aliekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe na wenzake waliovuliwa madaraka.

Viongozi wa Chadema wametakiwa kutekeleza agizo hilo ndani ya siku nne kuanzia jana.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Vijana wa Kanda ya Magharibi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Matawi ya Chadema, Mkoa wa Mwanza, Robert Gwanchele wakati akizungumza na waandishi wa habari Kwa mujibu wa Gwanchele,