
Ajali hii imetokea karibu kabisa na geti la chuo cha ardhi Jijini Dar Es Salaam.
Imehusisha gar aina ya costa iliyokuwa imebeba abiria wa kutoka makongo kwenda makumbusho.
Inasadikika kuwa aliyekuwa anaendesha gari hiyo sio dereva bali ni kuli.
Ajali imetokea wakati njemba hiyo ilipotaka kuingia barabara kubwa bila kupunguza mwendo(alitaka alale nayo).
Gari ilipoteza balance na
kuangukia upande wa kulia ambapo iliweza kugonga gari ingine aina ya Prado.
Abiria wameumia vibaya sana na waliweza kukimbizwa hospital haraka.

☆☆NJEMBA YAKIMBIA☆☆
Jamaa huyo baada ya kuangusha gari hiyo alijaribu kukimbia ambapo wanachuo pamoja na madereva boraboda.walimkamata na kuanza kumshushia kipigo lakin police walimuokoa.
☆☆☆KONDA ACHAPA LAPA☆☆☆
Wakati purukushani zinaendelea kondakta alipata upenyo na kutokomea pasipojulikana.
Tuendelee kuwaombea waliopo hospital ili hali zao zikae pouwa..
Imeripotiwa na David Mtengile Talented
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment