Saturday, 30 November 2013

MSAFARA WA MWENYEKITI UVCCM WAWEKEWA MAGOGO


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) taifa, Sadifa Juma Khamis (MB) Polisi mkoani Pwani inachunguza kundi la watu linalodaiwa kuweka magogo barabarani kuzuia msafara wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) taifa, Sadifa Juma Khamis (MB) katika eneo la Tondoroni, wilayani Kisarawe, mkoani humo. 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Ulrich Matei, alisema atazungumzia suala hilo baada ya  kupata  taarifa kamili. 
Kwa mujibu  wa watu walioshuhudia tukio hilo, kundi hilo liliweka magogo hayo jana usiku katika barabara ya kati ya eneo la Mpuyani katika njia panda ya barabara iendayo vijijini kuingia barabara kuu ya Morogoro. 
Mashuhuda wa tukio hilo walisema katika nyakati tofauti kundi hilo lilianza kuzuia msafara huo kwa kutaka kushinikiza dai la mgogoro wa mipaka kati ya eneo la Jeshi la Wananchi wa Ulinzi Tanzania (JWTZ) na makazi ya watu katika eneo la Tondoroni, wilayani humo. 

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Lindi ajiuzulu

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Lindi, Ally Chitanda, ametangaza kujiondoa katika nafasi hiyo akieleza kuchoshwa na uamuzi wa kikanda na kikabila unaoendelea ndani ya chama hicho.
Mbali na Uenyekiti, Chitanda  pia alikuwa  Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa na Katibu Ofisi ya Katibu Mkuu- Sekretarieti nafasi ambayo pia alitangaza kujiuzulu jana, lakini akaahidi kuendelea kuwa mwanchama mwaminifu wa Chadema.
Hata hivyo katika maelezo yake ya sababu za kujiuzulu alisema: “Sioni sababu ya kuendelea kuwa mwana Chadema, sioni sababu ya kuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Lindi.”
“Sioni sababu ya kuwa kiongozi kwa kuwa kipaumbele cha Chadema ni kukijenga chama Kaskazini, basi sisi wa Lindi tunawatakia kila la heri….”
Alisema amefikia hatua hiyo baada ya uamuzi wa Kamati Kuu ya Chama hicho, kuwavua nyadhifa Zitto na mwenzake Dk Kitila Mkumbo wiki iliyopita.

HIVI NDIVYO MSHINDI WA EBSS MWAKA HUU 2013 ALIVYOKABIDHIWA KITITA CHA MILIONI 50 ALFAJIRI YA LEO..! CHEKI HAPA



Zawadi kwa mshindi wa mwaka huu ni Milion hamsini[50]ambayo kakabidhiwa jukwaani.

 
Kinyanganyiro cha kumtafuta Super Star wa Bongo kupitia Epiq Bongo Star Search 2013 kimekamilika alfajiri hii kwenye ukumbi wa Escape 1.

 
Mashindano haya ambayo kidogo yalichelewa kuanza yalipambwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Barnaba,Makomando,Young Killer,water chilambo,Shaa,Kimbunga na Snura.

Katika mashindano haya ambayo yalikua na jumla ya washiriki watano ambao ni Amina Chibaba,Elizabeth Mwakijambile,Emmanuel Msuya,Maina Thadei na Melisa John,ambao walipita kwa round tatu kisha majaji kuwapunguza watatu na kisha kubakia Emanuel Msuya na Elizabeth Mwakijambile katika Round ya 4 na ya mwisho.


 
Katika round ya mwisho,Emmanuel Msuya ameibuka kidedea na kuwa Mshindi wa Epiq Bongo Star Search 2013,akiwa ni mshiriki anaetokea Jijini Mwanza na kumpokea taji water chilambo ambae alikua mshindi wa mwaka jana.

MCHEZAJI DAVID BECKHAM ANUNUA JUMBA LENYE THAMANI YA SH 77.5 BILLION ZA KITANZANIA ONA PICHA HAPA.


Beckham anunua jumba la kifahari lenye thamani ya £30million sawa na Tshs. 77,493,300,000.00 (Bilioni 77.5): The new Beckingham Palace: Four nail bars, a catwalk, even a waterfall - the secrets of the Beckhams' riotously naff new £30million London Home

Beckham anunua jumba la kifahari lenye thamani ya £30million sawa na Tshs. 77,493,300,000.00 (Bilioni 77.5): The new Beckingham Palace: Four nail bars, a catwalk, even a waterfall - the secrets of the Beckhams' riotously naff new £30million London Home.


Floor ya 3: ina bedroom 3 za wageni, sehemu ya pool table na baa ndogo. Floor ya 2: in master bedroom1 na master birthroom 1, pia ina sehemu ya manicure, hair dressing na make up na sehemu hii ni mfano wa theatre dressing room pia ina sehemu nzuri sana ya kupumzikia. Floor ya 1: ina Victoria’s dressing room, restaurant-standard kitchen, dinning room na family living room. Ground floor: ina offisi ya Victoria, mlango wa siri, study room, play room, store, powder Room. Lower ground floor: Luxury spa and GYM, store room 

David and Victoria Beckham are rumoured to have paid £30million for 'Beckingham Palace MkII' in Kensington & Chelsea and have put aside £5million for renovation



The grand facade of the Beckhams’ new London home has remained unaltered for 150 years, but its occupants over the decades tell a revealing story of social change.

One of its first residents in the 1880s was a successful Yorkshire wool broker. In the 1920s a Peruvian diplomat lived here, and in 1930 it became a boarding house for genteel single ladies.
By the 1990s, the dawn of a flashy new epoch was reflected in the installation of a vast subterranean pool complex beneath the house, which had been bought by a rich horse-breeder.
In 2005, a Guernsey-based holding company purchased the property and it is believed to have been unoccupied for several years.
This week its new owners were revealed to be Victoria and David Beckham, who intend to put their own unique imprint on the property.
When the retired footballer, his fashion designer wife and their four children move in, the house will once again take on a new hue — that of our celebrity-obsessed era.
The couple, who have been renting a property in Kensington since January, have, according to one source, paid more than £30 million for the house, which stands on one of the smartest streets in the Royal Borough of Kensington and Chelsea.
At more than 9,000 square feet, it is one of the largest in the area, boasting eight bedrooms and seven bathrooms.
Victoria, 39, has instructed the interior designer Kelly Hoppen — who is a friend — to renovate the house, with an upper budget of £5 million.

Wednesday, 27 November 2013

WAZIRI MKUU WA UKRAINE JULIA TYMOSHENKO AANZA MGOMO WA KUTOKULA CHAKULA NCHINI HUMO.

Waziri Mkuu wa zamani wa Ukraine, Julia Tymoshenko
Waziri Mkuu wa zamani wa Ukraine, Julia Tymoshenko.

KIONGOZI wa upinzani nchini Ukraine, Julia Tymoshenko leo ameanza mgomo wa kula chakula, akiwaunga mkono maelfu ya watu wanaopinga uamuzi wa serikali hiyo kuubatilisha mkataba baina ya nchi hiyo na Umoja wa Ulaya.


Tymoshenko, kiongozi mwenza wa muungano uliofanya mapinduzi yaliyopewa jina la chungwa, mwaka 2004, unaounga mkono mataifa ya Magharibi, alitangaza kuanza mgomo huo katika barua yake aliyowaandikia wafuasi wapatao 20,000 jana Jumatatu wanaounga mkono mkataba wa ushirikiano
kati ya Ukraine na Umoja wa Ulaya, ambao wanaandamana mjini Kiev kwa siku ya pili mfululizo.


Tymoshenko aliyekuwa waziri mkuu wa Ukraine, amesema ataendelea kugoma hadi hapo Rais Viktor Yanukovych atakaposaini mkataba huo kuhusu ushirikiano na biashara huru na Umoja wa Ulaya. 
Ameongeza kusema kuwa iwapo Yanukovych hatosaini mkataba huo tarehe 29 ya mwezi huu wa Novemba, atolewe katika uongozi wa Ukraine kwa njia ya amani na kikatiba, pamoja na wasaidizi wake wa kisiasa na wala rushwa.

Serikali yatangaza nafasi za kazi 2,748.

Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia watanzania wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 2,748 kwa ajili ya waajiri mbalimbali Nchini.
Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya waajiri mbalimbali wa Ofisi za Umma.
Daudi alitaja nafasi za kazi zinazotangazwa kuwa ni Afisa Uvuvi daraja la ii, Mvuvi msaidizi daraja la ii, Afisa Mifugo msaidizi daraja la ii, Afisa mifugo daraja la ii, Mteknolijia wa samaki daraja la ii, Daktari wa mifugo daraja la ii,Afisa utafiti Mifugo daraja la ii, Daktari utafiti Mifugo daraja la ii, Fundi sanifu Maabara Mifugo daraja la ii, Mkufunzi Mifugo daraja ii, Mkufunzi wa Mifugo msaidizi na Daktari Mifugo.

Kada nyingine ni Mkufunzi daraja la ii, Mtekinolojia wa Samaki msaidizi daraja la ii, uunda boti daraja ii, nafasi 2, Dereva wa vivuko daraja la ii, msaidizi mifugo,afisa kilimo daraja la ii, Afisa kilimo msaidizi daraja la ii, Mhandisi kilimo daraja la ii, Fundi sanifu daraja la ii, Afisa utafiti kilimo daraja la ii, Mkufunzi wa kilimo msaidizi, Afisa kilimo msaidizi daraja la iii,Dereva daraja la ii, mlinzi, Mhasibu mkuu daraja ii, Msanifu lugha mkuu iii na Afisa vipimo.

Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira nafasi hizo za kazi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kiteto, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mlele, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kalambo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mpanda, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nkasi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Sumbawanga na Mkurugenzi Manispaa ya Kinondoni.

Tuesday, 26 November 2013

SERIKALI YA ANGOLA YAZUIA DINI YA KIISLAM NA KUVUNJA MISIKITI YOTE.



WAKATI uhuru wa kuabudu upo kwa kila mtu, Angola inaonekana kupingana na jambo hili.  


Nchi hiyo ya kusini mwa Afrika inasemekana imekuwa nchi ya kwanza duniani kupiga marufuku dini ya Uislam ambapo kwa mujibu wa habari mbalimbali kutoka nchini humo, misikiti imefungwa na baadhi imeharibiwa.

Gazeti la Guardian liliripoti Novemba 22 mwaka huu kwamba Waziri wa Utamaduni wa Angola, Rosa Cruz e Silva, alisema “mchakato wa kuhalalisha Uislam haujapitishwa na Wizara ya Sheria na Haki za Binadamu, hivyo misikiti itafungwa hadi taarifa maalum itakapotolewa.”

 Waziri huyo alisema misikiti inafungwa ili kukomesha kinachoitwa kuzuia madhehebu haramu ya kidini ambapo chini ya sheria za nchi hiyo madhehebu mengi ya kidini yanachukuliwa kuwa ni ya kihalifu.

Mwezi huu tarehe 24,  Rais wa Angola, José Eduardo dos Santos, alisema nchi hiyo imo katika mchakato wa kukomesha taathira ya Uislam katika nchi hiyo ambapo Gavana wa Luanda, Bento Bento, alisema Waislam “wenye msimamo mkali” hawaruhusiwi  nchini humo na kwamba serikali ya Angola haitaruhusu kuwepo misikiti na nyumba zozote za ibada kwa Waislam.