Wednesday, 7 August 2013

UTOAJI WA MIMBA NI HATARI SANA KWA WANAWAKE




Utafiti mpya uliofanywa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii umeonyesha kuwa kutoboka kwa kibofu cha mkojo, kushamiri kwa kansa ya shingo ya uzazi, utasa na matatizo ya kisaikolojia kwa wanawake kunatokana na kasi kubwa ya utoaji mimba nchini. Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Mtumwa Mwako(pichani), akizungumza mjini hapa jana, alisema ripoti ya utafiti huo inaonyesha kwamba, utoaji mimba ndiyo  chanzo kikuu cha matatizo mengi kwa wanawake.

MADUDU YAFICHUKA KWENYE MTIHANI WA DARASA LA 7.

MBUNGE wa kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), ameibua madudu mapya katika sekta ya elimu, ambao umebaini kwamba kwenye mitihani ya majaribio ya darasa la saba, baadhi ya maswali ya kuchagua, hayakuwa na majibu.

Mitihani hiyo ya majaribio ya programu maalum ya matokeo makubwa sasa, kwa mujibu wa Mbatia ilifanywa na wanafunzi wa darasa la saba hivi karibuni katika masomo ya Hisabati, Kiswahili na Kiingereza katika wilaya 40 nchini.

MHADHIRI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (Patrick Rweyongeza) APIGWA RISASI NA KUFARIKI LEO HII JIJINI DAR

Patrick Rweyongeza, Mhadhiri (College of Engeneering) UDSM, ameuawa leo kwa kupigwa na risasi.

Tukio limetokea majira ya mchana maeneo Magomeni TANESCO wakati marehemu akielekea mjini ambapo watu waliokuwa
wamepakizana kwa pikpiki kumfuata na kumfyatulia risasi kisha kutokomea.

Haijafahamika kama kuna uporaji uliofanyika au la.

Tuesday, 6 August 2013

MAMA SALMA KIKWETE AWATAKA WANAWAKE NCHINI KUISHI MAISHA YA UPENDO

IMG_7532
Wanawake nchini wametakiwa kuishi maisha ya  upendo,
 umoja na mshikamano bila ya kuangalia itikadi zao za dini na
 vyama vya 
siasa hatua itakayosaidia kuimarisha hali ya amani na  utulivu.
Wito huo umetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete 
wakati wa futari ya pamoja aliyoiandaa kwa ajili ya wanawake 
viongozi  na  wake wa viongozi  Ikulu jijini Dar es Salaam .

AJALI MBAYA YATOKEA MBEYA MMOJA AFARIKI PAPO HAPO


GARI AINA YA TOYOTA COROLLA  ILIYOGONGANA NA BASI 
LA HOOD MENEO YA MSWISWI MBEYA DEREVA
 WA GARI NDOGO AMEFARIKI PAPO HAPO
HATI YA KUSAFIRIA YA MAREHEMU DAVIS HANAMUNDE MZAMBIA




MNAMO TAREHE 04.08.2013  MAJIRA YA SAA 06:45HRS HUKO MSWISWI 

WILAYA YA MBARALI BARABARA YA MBEYA/IRINGA, GARI NO T. 159 AXM 
AINA YA SCANIA BUS MALI YA KAMPUNI YA   HOOD LIKIENDESHWA NA
 DEREVA OMARY  SAID, MIAKA 50, MZIGUA, MKAZI WA MABIBO DSM LILIGONGANA NA GARI NO IT.3014 TOYOTA COROLLA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA DEVIS  ANAMUNDE, MIAKA 28, MZAMBIA
 MKAZI WA MUNZE LUSAKA NA KUSABABISHA KIFO CHA DEREVA HUYO 
PAPO HAPO.

MAUAJI ; VIKONGWE VYAUWAWA KIKATILI KWA IMANI ZA KISHIRIKINA MKOANI LINDI

clip_image002Vikongwe wawili wakazi wa Kata za Rutamba na Mingoyo mkoani Lindi, wameuawa kwa kushambuliwa kwa silaha mbalimbali, ikiwamo jembe na mapanga kwa madai ya imani za kishirikina.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani hapa, George Mwakajinga, vikongwe haowaliuawa Julai 29 na 30 mwaka huu, saa 9:30 na 10:30 alasiri.

Mwakajinga amewataja marehemu hao kuwa ni, Esha Mohamedi (81) mkulima wa kijiji cha Kinyope, Kata ya Rutamba, Lindi Vijijini na Mary Albert (61) wa kata ya Mingoyo, Manispaa ya Lindi.