Uthibitisho
huu umetoka kwa mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Mitihani Tanzania
(NECTA) Brof Rwekaza Mukandala kuwa Katibu Mtendaji wa NECTA Dr Joyce
Ndalichako ameondoka NECTA na nafasi yake sasa inakaimiwa na Dr Charles
Msonde aliyekuwa msaidizi wake. Kwa
mujibu wa Profesa Mukandala, ni kwamba Dr Ndalichako ameanza likizo ya
utafiti (Sabbatical leave) ya mwaka mmoja kuanzia Oktoba mosi mwaka huu
hadi Septemba 30 mwaka 2014 licha ya kuwepo kwa taarifa za kuwepo
shinikizo la kisiasa lilikuwa likimzonga Dr Ndalichako kutakiwa
kujiuzulu.
No comments:
Post a Comment