MZEE MAJUTO WA BONGO MOVIE ATANGAZE KUGOMBEA UBUNGE MWAKA 2015 JIMBO LA TANGA MJINI
King Majuto
MCHEKESHAJI mkongwe nchini, Amri Athuman 'King Majuto' ametangaza nia
yake ya kujitosa kwenye siasa akitaka kuwania Ubunge katika Jimbo la
Tanga Mjini katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015. Akihojiwa na kituo cha Clouds FM, Mzee Majuto mwenye umri zaidi ya miaka
60, alisema Mungu akimjalia atajitosa kwenye ubunge jimboni humo
kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), akidai kiu hiyo imechochewa na
mafanikio ya wasanii waliojitosa kwenye siasa na kufanya vyema.
Yekonia
Mzee Majuto alisema, uzoefu alionao katika kuishi kwake mjini Tanga
itamwezesha kuwatatulia kero na kuwaletea maendeleo ya kweli wananchi
wenzake iwapo Mungu atamjalia katika kusudio lake.
Kadhalika Muigizaji, ambaye pia ni mtayarishaji na muongozaji wa filamu
nchini, Yekonia Watson 'Amani' amesema matarajio yake miaka michache
ijayo ni kujitosa kwenye siasa akitaka kuwania Ubunge kabla ya kuangalia
nafasi ya juu zaidi kwa maana Rais.
Akizungumza na PAPARAZI jioni hii, Watson alisema anaamini ana uwezo na
kipawa cha uongozi hivyo anaweka mambo sawa kabla ya kujitosa jumla
kwenye duru hilo, japo yeye hakuweka bayana atajitosa kupitia chama
gani.
"Kwa sasa ni mapema mno, ila nitaanzia Ubunge kisha kuangalia nafasi ya
juu, ila muhimu Mungu anipe uhai na umri wa kufanikisha hilo," alisema
mkali huyo anayejiandaa kuachia filamu yake mpya iitwayo 'Uwanja wa
Vita' aliyoigiza na wasanii kadhaa nyota akiwamo Irene Uwoya
No comments:
Post a Comment